May 06, 2024 04:39 UTC
  • Polisi waondoa kambi ya waungaji mkono wa Palestina katika Chuo Kikuu cha California Kusini

Polisi wa Los Angeles huko Marekani wameondoa kambi ya watu wanaoiunga mkono Palestina pambizoni mwa uwanja wa chuo kikuu cha California kusini.

 

Shirika la habari la (IRNA) limetoa ripoti kwamba, makumi ya maafisa kutoka Idara ya Polisi ya Los Angeles huko Marekani (LAPD) walifika chuoni hapa na kuzuia kuingia na kutoka kwa wanafunzi wanaounga mkono Palestina katika chuo kikuu hicho.

Maafisa wa  polisi wa Chuo Kikuu cha California Kusini waliwataka wanafunzi wanaounga mkono Palestina kuondoka katika eneo hilo haraka iwezekanavyo la sivyo wakamatwe.

Katika wiki chache zilizopita, wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani wamekuwa wakifanya maandamano makubwa wakitaka kusitishwa vita haraka na kikamilifu huko ukanda wa Gaza na kusitishwa kwa uwekezaji wa vyuo vikuu vyao katika makampuni yanayounga mkono utawala haramu wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari katika ukanda huo.

Zaidi ya watu  elfu 2,300 wamekamatwa katika maandamano ya watu wanaiunga mkono Palestina katika vyuo vikuu hivyo kote nchi  Marekani.

Jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina huko Gaza zimewakasirisha sana walimwengu na kuzipelekea serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa kutoa wito wa kutetewa wananchi madhulumu na wasio na ulinzi wa ukanda wa Gaza.

Waungaji mkono wa Wapalestina duniani wamelaani vitendo vya jinai vya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza kwa kufanya maandamano katika nchi nyingi za dunia, ikiwemo Marekani, katika miezi ya karibuni.

Tags