Apr 23, 2024 08:24 UTC
  • Safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan

Ziara ya siku mbili ya Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan inatathminiwa kuwa ni safari ya kihistoria ambayo inatarajiwa kufungua ukurasa na anga mpya ya uhusiano kati ya Tehran na Islamabad.

Kupokewa kwa wigo mpana safari hii na duru mbalimbali za umma, kisiasa na hata kiuchumi za Pakistan kunachukuliwa kuwa kielelezo tosha cha kupokewa pakubwa safari hii nchini Pakistan na kuhesabiwa kuwa itapelekea kufunguliwa ukurasa mpya wa mahusiano kati ya pande hizo mbili. Wanasiasa na wakuu wa vyama vya siasa nchini Pakistan sambamba na kukkaribisha kwa mikono miwili safari ya Ebrahim Raiisi nchini Pakistan walitangaza azma yao ya kuunga mkono kustawisha uhusiano kati ya nchi mbili hizi.

Kwa muda wa takribani wiki mbili zilizopita, duru za kisiasa na vyombo vya habari vya Pakistan sanjari na kuzungumzia safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Islamabad, ziliitathmini safari hi kuwa ni hatua ya kuleta mageuzi katika uhusiano kati ya pande hizo mbili. Hasa kwa kutilia maanani kwamba, lengo la safari hii ni kupanua na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara, mazungumzo ya pande mbili na mashauriano ya kikanda.

Kwa kuzingatia kuwa, siasa za kimsingi za serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kustawisha uhusiano na nchi jirani, katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kiwango cha uhusiano kati ya Tehran na Islamabad kimestawi kwa kiasi kikubwa, na kiasi cha mabadilishano ya kibiashara kimepanda na kuwa maradufu na kufikia dola bilioni mbili nusu katika mwaka uliopita.

Rais Ebrahim Raisi akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif

 

Abbas Fayaz, mweledi wa masuala ya kisiasa anasema kuhusiana na suala hili kwamba: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan, mbali na kuwa nchi mbili jirani za Kiislamu, zina mambo zinayoshabihiana kiutamaduni, kidini na hata kilugha, na lugha ya Kifarsi ni miongoni mwa lugha pendwa, maarufu na yenye wafuasi wengi nchini Pakistani na huko nyuma ilikuwa ikihesabiwa kuwa moja ya lugha rasmi katika nchi hiyo.

Fauka ya hayo, wananchi wa Pakistan wanatilia maanani sana suala la kushiriikiana na Iran ambapo kilele cha hilo tulikishuhudia katika mapokezi ya kihistoria ya ziara ya Kiongozi Muadhamu Ayatullah Ali Khamenei nchini Pakistan katika kipindi ambacho alikuwa Rais wa Iran. Kustawishwa uhusiano wa Iran na Pakistan kunaweza kufanywa katika nyuga pana za kiuchumi, kibiashara uwekezaji ambapo kwa kutambua fursa na majukwaa mengi kadiri inavyowezekanavyo, tunaweza kushuhudia kuongezeka ustawi unaoongezeka wa ushirikiano. Hasa kwa kutilia maanani kwamba, kiwango cha mabadilishano ya kibiashara si cha kuridhisha ikilinganishwa nyanja na fursa zilizopo baina ya mataifa haya mawili ya Kiislamu.

Kuhusu upanuzi wa biashara ya kikanda na uwekezaji huko Makran, Gwadar na Chabahar, licha ya kauli za uchochezi na zenye malengo maalumu za duru za kigeni, maeneo haya sio tu hayakabiliani, lakini yanakamilishana kwa minajili ya maendeleo ya kikanda. Mbali na kupanua ushirikiano katika sekta za kiuchumi na kibiashara, Iran na Pakistan zina misimamo mingi ya pamoja kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa, ambayo inaweza kuwa sababu athirifu ya kubadilisha milingano mingi ya kupandikiza iliyowekwa na nchi za Magharibi.

Safari ya Raiis wa Iran nchini Pakistan

 

Miongoni mwa mambo ambayo Iran na Pakistan zinashirikiana ni suala la kulihami na kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina dhidi ya jinai za kila uchao na zinazoongezeka za utawala wa Kizayuni, ambapo serikali na wananchi wa Pakistan daima wamekuwa mstari wa mbele katika uwanja huu.

Hapana shaka kuwa kujiamini kwa nchi za Kiislamu katiika kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel kunaweza kusaidia kutatua matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu hususan kadhia ya Palestina.

Radiamali ya kuadhibu na kutia adabu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupitia Operesheni ya Ahadi ya Kweli dhidi ya utawala wa Kizayuni unaoua watoto si tu kwamba imesambaratisha nguvu bandia za utawala huo dhalimu, bali hilo limewadhihirishia walimwengu pia ya kwamba, ulimwengu wa Kiislamu una uwezo na nguvu nyingi za kulinda malengo matukufu ya wananchi wa Palestina.

Kwa muktadha huo, ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Pakistan ni hatua muhimu katika kusaidia kuimarisha umoja na udugu wa nchi za Kiislamu ili kulinda adhama na mamlaka ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya ubeberu wa kimataifa.

Ni kutokana na sababu hiyo, ndio maana wananchi wa Pakistan wanataraji kuiona serikali yao ikiwa pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuchukua hatua za kivitendo za kuimarisha zaidi ushirikiano ukiwemo wa sekta ya nishati na pia kuimarisha kambi ya muqawama dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Kizayuni na hivyo kuonyesha kuwa, ipo pamoja na muqawama dhidi ya wavamizi wa Kizayuni.

Tags