-
Maher Hamoud: Katika miaka 40 iliyopita Palestina imekuwa kadhia muhimu kwa Iran
Feb 09, 2019 21:46Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Muqawama amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita Iran imeheshimu na kushikamana na misingi yake ya thamani ikiwemo kuiunga mkono Palestina.
-
Iran yasisitiza udharura wa kuwa na uhusiano mwema na nchi zote duniani
Feb 09, 2019 13:44Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kislamu ya Iran imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 40 wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kusisitiza kuwa: Kuwa na uhusiano wa heshima, wa amani na wa pande kadhaa na nchi za dunia ni miongoni mwa stratijia za Iran.
-
Palestina yasema haitashiriki mkutano wa Marekani wa Warsaw
Feb 09, 2019 04:10Palestina imesema licha ya kupokea mwaliko, lakini haitahudhuria mkutano wa hapo tarehe 13 na 14 mwezi huu wa Februari huko Warsaw mji mkuu wa Poland, uliopewa anwani ya "Mkutano wa Amani na Usalama katika Mashariki ya Kati".
-
Iran Itaendelea na shughuli zake za makombora ya kujihami
Feb 09, 2019 00:17Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu matamshi yasiyo na msingi ya watawala wa Marekani kuhusu mpango wa Iran wa kurusha satalaiti katika anga za mbali na makombora na kusema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitafanya mazungumzo kuhusu makombora yake ya kujihami.
-
Kiongozi Muadhamu: Maadhimisho ya mwaka huu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yatakuwa ya hamasa zaidi
Feb 08, 2019 11:19Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kwa kuwa macho wananchi na kwa mahudhurio ya watu wenye mitazamo tofauti maadhimisho ya mwaka huu ya 22 Bahman ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yatakuwa makubwa na ya hamasa zaidi ikilinganishwa na ya huko nyuma.
-
Baqeri: Vitisho havitaishurutisha Iran ifanye mazungumzo kuhusu uwezo wake wa makombora
Feb 07, 2019 19:08Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vitisho vya adui haviwezi kuifanya Iran isalimu amri na kusitisha jitihada zake za kustawisha uwezo wake wa makombora.
-
Vyombo vya habari Marekani: Fikra za Trump kuhusu Iran hazina mlingano, zinafurutu mipaka
Feb 06, 2019 23:27Vyombo vya habari vya Marekani vimetangaza kuwa, matamshi yanayotolewa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo yanaonesha kuwa, kiongozi huyo ana mitazamo na fikra zisizo na mlingano na za kuchupa mipaka kuhusiana na Iran.
-
Onyo la Iran kwa chokochoko za Israel dhidi ya Syria
Feb 06, 2019 03:34Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa nchini Iran ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya kuendelea kuishambulia Syria.
-
Rais Rouhani: Zama za Marekani kuitawala Iran haziwezi kurejea
Feb 05, 2019 23:44Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulaani misimamo ya uhasama ya Marekani kwa Iran tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu miaka 40 iliyopita, amesema zama za Washington kuishurutisha na kuitawala Iran zimekwisha na katu haziwezi kurejea.
-
Larijani: Uchaguzi Iran ni hazina muhimu ya demokrasia ya kidini
Feb 05, 2019 23:13Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameutaja uchaguzi hapa nchini kama hazina muhimu ya demokrasia ya kidini.