Feb 06, 2019 02:43 UTC
  • Larijani: Uchaguzi Iran ni hazina muhimu ya demokrasia ya kidini

Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameutaja uchaguzi hapa nchini kama hazina muhimu ya demokrasia ya kidini.

Dakta Ali Larijani alisema hayo jana bungeni na kuongeza kuwa, wananchi wa Iran wana fursa ya kuwachagua viongozi wao moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia uchaguzi.

Amesema uchaguzi ni mtaji mkubwa wa kisiasa na kijamii unaopaswa kulindwa kwa nguvu zote, na kwamba Mapinduzi ya Kiislamu yaling'oa mizizi ya ubeberu wa Marekani na kutuma ujumbe mzito kwa madikteta wa eneo hili.

Amesema kitendo hicho cha Wairani kuwa na fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka ni katika mafanikio makubwa ya Mapinduzi ya Kiisamu ya Iran ambayo yana umri wa miaka 40 sasa.

Wananchi wa Iran wakiwa katika harakati ya Mapinduzi ya Kiislamu 1979

Kadhalika Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha kuwa, Mapinduzi ya Kiisamu ya Iran yaliyopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Khomeini MA lilikuwa tukio kubwa la kihistoria.

Amesisitiza kuwa, wananchi wanamapiduzi wa Iran walifanya kazi kubwa ya kihistoria mnamo Februari mwaka 1979, na hatimaye wakapata ushindi mkubwa na kuuangusha utawala wa kidkteta.

Tags