Maher Hamoud: Katika miaka 40 iliyopita Palestina imekuwa kadhia muhimu kwa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51445-maher_hamoud_katika_miaka_40_iliyopita_palestina_imekuwa_kadhia_muhimu_kwa_iran
Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Muqawama amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita Iran imeheshimu na kushikamana na misingi yake ya thamani ikiwemo kuiunga mkono Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 09, 2019 21:46 UTC
  • Maher Hamoud: Katika miaka 40 iliyopita Palestina imekuwa kadhia muhimu kwa Iran

Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Muqawama amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka 40 iliyopita Iran imeheshimu na kushikamana na misingi yake ya thamani ikiwemo kuiunga mkono Palestina.

Sheikh Maher Hamoud amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanatimiza mwaka wake wa arubaini na kuuingiza Ulimwengu wa Kiislamu katika awamu na kipindi kipya cha mafanikio mengi. Sheikh Hamoud amesema kuwa kaulimbiu ya kukabiliana na siasa za Marekani na kuuangamiza utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati haiihusu Iran pekee na kueleza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu imethibitisha kuwa siasa za Marekani ambazo zilikuwa na lengo la kuisambaratisha Iran, zimefeli

Akiwa katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha kumbukumu za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Ayatullah Khamenei mjini Beirut, Sheikh Ali Damush Naibu Mkuu wa Baraza la Utekelezaji la harakati ya Hizbullah ya Lebanon pia  ameeleza kuwa Iran imepata mafanikio makubwa katika nyanja zote kutokana na busara za Kiongozi Muadhamu, kuwa na subira na kutolegalega taifa hilo. 

Sheikh Ali Damush, Naibu Mkuu wa Baraza la Utekelezaji la Harakati ya Hizbullah ya Lebanon 
 

Sheikh Damush amesisitiza kuwa, kushindwa Marekani, Israel na waitifaki wake katika eneo la Mashariki ya Kati na kupata ushindi mhimili wa muqawama huko Iraq, Syria, Yemen, Palestina na Lebanon ni matokeo ya uongozi wa busara, kusimama kidete na mapambano ya mataifa ya eneo hili.

Kipindi cha kuanzia tarehe 12 mwezi Bahman yaani siku aliyowasili nchini Iran Imam Khomeini (M.A) hadi tarehe 22 Bahman sawa na Februari 11 ambayo ni siku ya Ushindi ya Mapinduzi ya Kiislamu kimepewa jina la "Alfajiri Kumi" na kila mwaka hufanyika sherehe maalumu katika kipindi hicho.