-
Pezeshkian: Mipaka ya kijiografia kamwe haiwezi kuyatenganisha mataifa mawili ndugu ya Iran na Iraq
Sep 08, 2025 04:06Rais wa Iran ameutaja uhusiano kati ya mataifa mawili na nchi mbili za Iran na Iraq chini ya kivuli cha mifungamano ya kidini na kiutamaduni kuwa mkubwa na wa kihistoria na kusisitiza kuwa mipaka ya kijiografia kamwe haiwezi kutenganisha mataifa haya mawili ndugu.
-
Araghchi: Iran na IAEA zinakaribia kuunda fremu mpya ya ushirikiano
Sep 06, 2025 23:20Iran imesema imekaribia sana kubuni mfumo mpya wa ushirikiano baina yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), miezi kadhaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii kuipelekea Tehran kusimamisha ushirikiano wake na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Jeshi la Majini la Iran lipo Afrika Kusini kujadili luteka ijayo ya BRICS
Sep 06, 2025 08:31Mkutano wa kujadili mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya baharini ya nchi wanachama wa BRICS umefanyika katika mji bandari wa Cape Town nchini Afrika Kusini, kwa kushirikisha wawakilishi kutoka nchi sita, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Sambamba na kuanza duru mpya ya mazungumzo, Iran yatilia mkazo diplomasia katika kadhia ya nyuklia
Sep 06, 2025 03:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa liidhinishe juhudi za kidiplomasia katika kushughulikia mpango wa nyuklia wa Tehran na kukomesha vitendo vya "kinyume na sheria" vya Ulaya.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa
Sep 05, 2025 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema, mazungumzo yake na viongozi wa Qatar yalikuwa yenye faida na mafanikio makubwa na yalifanyika kwa uzito maalumu na akaongezea kwa kusema: "kwa bahati nzuri, hakuna tofauti zozote kati ya nchi hizi mbili, na sutafahamu iliyojitokeza imetatuliwa kikamilifu na ziara hii".
-
Iran yaitaka dunia ilaani mashambulizi dhidi ya vituo vyake vya nyuklia
Sep 05, 2025 07:32Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran amesema Marekani na utawala wa Israel zilifanya mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya vituo vya nyuklia ya Iran, licha ya vituo hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Nyuklia.
-
Araqchi: IAEA imeafiki haja ya mfumo mpya wa ushirikiano na Iran
Sep 04, 2025 22:49Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa hakutakuwa na ushirikiano mpya baina ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hadi hapo mazungumzo yatakapokamilika.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Jumuiya ya Shanghai inaweza kuasisi miungano ya usalama yenye ufanisi
Sep 04, 2025 10:33Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ina uwezo wa kupanua wigo wa shughuli zake na kuanzisha miungano ya usalama yenye ufanisi katika siku zijazo.
-
Araghchi: Iran haiogopi mazungumzo, wala vita
Sep 04, 2025 04:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu haiogopi kuingia katika mazungumzo mapya kuhusu utatuzi wa masuala yoyote yaliyopo, kama ambavyo haina hofu ya kuingia katika vita vyovyote vipya ambavyo vinaweza kutwishwa nchi hii na maadui zake.
-
Marekani inafutilia nini katika kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran?
Sep 04, 2025 03:51Marekani imeweka vikwazo vipya ili kuzuia uuzaji nje wa mafuta ya Iran.