-
75% ya Waisrael wanaamini Netanyahu ameshindwa kukabiliana na Hizbullah
Aug 24, 2024 11:08Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya habari ya Mako ndani ya jamii ya Wazayuni yanaonyesha kuwa asilimia 75 ya Waisraeli hawaridhishwi na namna serikali ya waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu inavyoshughulikia hali ya usalama kwenye mpaka wa kaskazini, ambako kila siku kunaandamwa na mashambulio makali ya Harakati ya Muqawama wa Kiisilamu ya Hizbullah ya Lebanon tangu Israel ilipoanzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza Oktoba 7, 2023.
-
Muqawama Iraq: Jibu la Iran dhidi ya Israel litakuwa la nguvu
Aug 15, 2024 02:46Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya al-Nujabaa ya Iraq amesema jibu tarajiwa la Iran kwa mauaji ya kigaidi yaliyofanywa mwezi uliopita na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ismail Haniyah, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS litakuwa la nguvu, lenye taathira na la kimahesabu.
-
Ayatullah Khamenei: Kipaumbele muhimu ni utekelezaji wa makubaliano kati ya Iran na Iraq
Jul 31, 2024 03:36Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Iraq kwamba utekelezwaji wa mapatano baina ya nchi hizo mbili ndio kipaumbele muhimu zaidi.
-
Duru mpya ya mazungumzo ya pamoja ya usalama kati ya Marekani na Iraq mjini Washington
Jul 24, 2024 11:14Alina Romanowski, balozi wa Marekani mjini Baghdad, alitangaza siku ya Jumatatu kuhusu kuanza mazungumzo kati ya Marekani na Iraq huko Washington mji mkuu wa Marekani ajenda kuu ikiwa ni "mustakabali wa muungano wa kimataifa."
-
Iran iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya magendo ya madawa ya kulevya
Jul 24, 2024 02:37Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema katika kikao cha Mkutano wa Pili wa Kikanda wa Kupambana na Madawa ya Kulevya huko Baghdad kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kikamilifu kushirikiana na taasisi na mifumo ya kikanda na kimataifa kuendesha vita dhidi ya mihadarati.
-
Vikosi vya Yemen na Iraq vyafanya operesheni za kuitetea Palestina
Jul 16, 2024 07:18Vikosi vya wanamaji na vya makombora vya Yemen vimefanya operesheni nyingine dhidi ya meli za mafuta zilizokuwa zikielekea katika bandari za utawala wa Kizayuni unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.
-
Iran: Waliounga mkono mpango wa silaha za kemikali wa Saddam washtakiwe
Jul 11, 2024 13:22Balozi wa Iran nchini Uholanzi amesisitiza juu ya udharura wa kushtakiwa na kuadhibiwa waungaji mkono wa kigeni wa mpango wa silaha za kemikali wa utawala wa Baath wa Iraq uliokuuwa ukiongozwa na Saddam Hussein.
-
Rais mteule wa Iran na Rais wa Iraq watilia mkazo kustawisha uhusiano wa pande mbili
Jul 09, 2024 12:28Rais mteule wa Iran amezungumza kwa simu na Rais wa Iraq ambapo wamesisitiza udharura wa kustawisha uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.
-
Wanaharakati wa Iraq waipiga tena kwa makombora bandari ya Eilat ya utawala wa Kizayuni
Jul 01, 2024 08:07Wanaharakati wa Muqawama wa Iraq wamesema kuwa wamefanya shambulizi jipya dhidi ya Bandari ya Eilat katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu Wazayuni na ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.
-
Iran: Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kutumia suhula zote ili kusitisha jinai za Wazayuni Gaza
Jun 13, 2024 12:07Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Iran haitawaruhusu wavamizi wa Kizayuni kudhoofisha uthabiti na usalama wa eneo hata kwa chembe moja.