75% ya Waisrael wanaamini Netanyahu ameshindwa kukabiliana na Hizbullah
Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya habari ya Mako ndani ya jamii ya Wazayuni yanaonyesha kuwa asilimia 75 ya Waisraeli hawaridhishwi na namna serikali ya waziri mkuu wa utawala huo Benjamin Netanyahu inavyoshughulikia hali ya usalama kwenye mpaka wa kaskazini, ambako kila siku kunaandamwa na mashambulio makali ya Harakati ya Muqawama wa Kiisilamu ya Hizbullah ya Lebanon tangu Israel ilipoanzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza Oktoba 7, 2023.
Aidha, jumla ya asilimia 59 ya waliohojiwa wameonyesha kuunga mkono kufikia makubaliano na harakati ya Hamas ili kuwarejesha nyumbani mateka wa Israel, ikilinganishwa na asilimia 21 tu waliosema wanapinga mpango huo katika hali yake ya sasa, na wengine asilimia 20 ambao wamesema hawajui nini hasa kifanyike.