Vikosi vya Yemen na Iraq vyafanya operesheni za kuitetea Palestina
(last modified 2024-07-16T07:18:29+00:00 )
Jul 16, 2024 07:18 UTC
  • Vikosi vya Yemen na Iraq vyafanya operesheni za kuitetea Palestina

Vikosi vya wanamaji na vya makombora vya Yemen vimefanya operesheni nyingine dhidi ya meli za mafuta zilizokuwa zikielekea katika bandari za utawala wa Kizayuni unaokalia ardhi za Palestina kwa mabavu.

Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema vikosi vya nchi hiyo vimeshambulia kwa makombora ya balestiki na droni kadhaa meli ya mafuta yenye jina la ‘Chios Lion’ katika maji ya Bahari Nyekundu, ikielekea katika bandari ya Eilat, kwa ajili ya kuwaunga mkono Wapalestina wanaodhulumiwa huko Gaza

Saree amesema vikosi vya Yemen vimefanya pia operesheni ya pamoja ikishirikiana na Muqawama wa Kiislamu wa Iraq na kulenga meli ya “Olvia" ya kubebea bidhaa za mafuta na kemikali na nyingine ya Bentley zikiwa zimetia nanga katika bandari za Ashdod na Haifa, kabla ya hazijaelekea mashariki mwa Bahari ya Mediterraenia.

Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema wanajeshi wa Yemen wataendelea na operesheni zao za kijeshi, na watazuia meli zinazomilikiwa na Israel au zile zinazoelekea katika bandari zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu hadi pale usitishaji vita wa kudumu utakapotekelezwa katika Ukanda wa Gaza.

Shughulizi zimekuwa zikisuasua katika bandari ya Eilat kutokana hujuma za muqawama

Wakati huo huo, wanaharakati wa Muqawama wa Iraq wamesema kuwa wamefanya shambulizi jipya dhidi ya Bandari ya Eilat katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

Wanamuqawama wa Iraq wameeleza kuwa, wameshambulia Bandari ya Eilat kwa kutumia ndege zisizo na rubani aina ya kamikaze na makomboa ya ya cruise ya Arqab. Wanajihadi hao wa Muqawama wa Iraq wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya maeneo ya Israel tangu utawala huo unaoukalia kwa mabavu ardhi ya Palestina ulipoanzisha vita vya mauaji ya halaiki huko Ukanda wa Gaza mapema mwezi Oktoba 7, mwaka jana 2023.

Tags