-
Utafiti: Marekani na Israel ndio tishio kuu kwa Waarabu
Jul 13, 2018 03:11Utafiti mpya wa maoni unaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya Waarabu wanaitazama Marekani na utawala haramu wa Israel kama tishio kuu kwa usalama wa mataifa yao.
-
UN: Israel imebomoa nyumba 197 za Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Jul 11, 2018 23:40Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema utawala wa Kizayuni wa Israel umebomoa nyumba 197 za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu wa 2018.
-
Iran: Washauri wetu wa kijeshi kusalia Syria kuzima chokochoko za Israel
Jul 08, 2018 09:41Mshauri wa Masuala ya Kimataifa wa Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, washauri wa kijeshi wa Iran watasalia nchini Syria kuisaidia nchi hiyo ya Kiarabu kuzima chokochoko za mabaki ya magenge ya kigaidi yanayoungwa mkono na nchi ajinabi.
-
Wanafikra wa Kiarabu wakasirishwa na mwandishi wa Saudia aliyetaka kuimarishwa uhusiano na Israel
Jul 07, 2018 21:56Weledi wengi wa Kiarabu wamepatwa na hasira kali kufutia pendekezo la mwandishi mmoja wa Saudi Arabia, aliyeitaka serikali ya nchi hiyo kupanua mahusiano yake na utawala khabithi wa Kizayuni.
-
Jeshi la Syria lakomboa vijiji zaidi vilivyokuwa vimetekwa na magaidi wa ISIS mkoani Daraa
Jul 06, 2018 22:50Jeshi la Syria limewatimua magaidi na kukomboa kikamilifu vijiji kadhaa katika mkoa wa kusini magharibi wa Daraa karibu na mpaka wa Jordan kwa lengo la kufungua kituo cha kistratijia cha Nasib.
-
UN, EU zaitaka Israel isibomoe kijiji cha Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Jul 05, 2018 09:38Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe mpango wake wa kubomoa kijiji cha Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Jeshi la Israel lashambulia maandamano ya wanawake wa Kipalestina, 134 wajeruhiwa
Jul 04, 2018 02:57Askari katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameyashambulia kwa risasi hai maandamano ya wanawake wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza na kujeruhi 134 miongoni mwao.
-
Walimu wa sekondari Tunisia wakataa kusahihisha mtihani wakipinga Israel
Jul 03, 2018 23:21Walimu wa wa Tunsia wamepinga vikali mtihani wa historia na jografia ulioitambua Israel kuwa ni "dola" badala ya utawala vamizi na wamekataa kusahihisha mtihani huo.
-
Hizbullah: Shambulizi lolote la Israel dhidi ya Lebanon litajibiwa kwa kuteketeza eneo la Golan
Jul 03, 2018 03:05Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon sambamba na kuashiria onyo kali lililotolewa na Ufaransa kwa utawala haramu wa Kizayuni, imesema kuwa chokochoko yoyote ya Israel itakayofanywa dhidi ya Lebanon, itapelekea kuteketezwa eneo la milima ya Golan inayodhibitiwa na Israel kwa sasa.
-
Haaretz: Bahrain inataka kuanzisha uhusiano wa dhahiri na Israel
Jul 02, 2018 09:55Gazeti la Kizayuni la Haaretz limeashiria uhusiano wa siri kati ya utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain na utawala ghasibu wa Israel na kufichua kwamba, viongozi wa Manama wanataka kuanzisha uhusiano wa dhahiri na Tel-Aviv.