Utafiti: Marekani na Israel ndio tishio kuu kwa Waarabu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46747-utafiti_marekani_na_israel_ndio_tishio_kuu_kwa_waarabu
Utafiti mpya wa maoni unaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya Waarabu wanaitazama Marekani na utawala haramu wa Israel kama tishio kuu kwa usalama wa mataifa yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 13, 2018 03:11 UTC
  • Utafiti: Marekani na Israel ndio tishio kuu kwa Waarabu

Utafiti mpya wa maoni unaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya Waarabu wanaitazama Marekani na utawala haramu wa Israel kama tishio kuu kwa usalama wa mataifa yao.

Asilimia 90 ya waliohojiwa kwenye utafiti huo aidha wanasema utawala wa Kizayuni wa Israel ndilo chimbuko la ukosefu wa uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati.

Utafiti huo uliofanywa na shirika la Arab Center for Research and Policy Studies lenye makao yake mjini Doha, Qatar umebainisha kuwa, aghalabu ya wananchi wa nchi za Kiarabu wanaitazama kadhia ya Palestina kama suala linalowahusu wao zaidi.

Matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa kwenye tovuti ya Middle East Eye (MEE) yanaonesha kuwa, asilimia 81 ya raia 18,000 wa asili katika nchi 11 za Kiarabu waliohojiwa hawaungi mkono hatua ya watawala wao ya kuutambua utawala wa Kizayuni wa Israel.

Maandamano ya Wapalestina dhidi ya Israel

Kadhalika asilimia 87 ya waliohojiwa wanasema wana mtazamo hasi juu ya sera za Marekani dhidi ya Palestina. 

Kutokana na siasa kandamizi za Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia, Muhammad Bin Salman, asilimia 36 ya Wasaudia waliohojiwa waliogopa kueleza misimamo yao, ikilinganishwa na asilimia 5 katika nchi nyingine 10 zilizoshirikishwa kwenye utafiti huo.