Walimu wa sekondari Tunisia wakataa kusahihisha mtihani wakipinga Israel
Walimu wa wa Tunsia wamepinga vikali mtihani wa historia na jografia ulioitambua Israel kuwa ni "dola" badala ya utawala vamizi na wamekataa kusahihisha mtihani huo.
Makumi ya walimu wa shule za sekondari wamekusanyika katikati ya mji wa Ghasrin na kupaza sauti zao za kupinga hatua yoyote ya kuitambua Israel kama dola na nchi. Walimu hao wamesema kuwa, hawatasahihisha mtihani huo maadamu unautaja utawala huo katili kuwa ni dola na nchi.
Msemaji wa walimu hao amesema kuwa, jina la Israel linapaswa kuandamana na sifa ya utawala ghasibu, katili na wa kizayuni katika fikra za wanafunzi wa Tunisia na kwamba kadhia ya taifa la Palestina ina umuhimu mkubwa kwa Watunisia.
Ameongeza kuwa Tunisia haijaitambua Israel kuwa ni nchi tangu ilipoivamia na kuikalia ardhi ya Palestina mwaka 1947.
Katika miaka ya hivi karibuni Israel imezidisha harakati za kubomoa nyumba za raia wa Palestina na kuharibu mashamba yao na kisha kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuhi mahala pake.