-
Zarif aitaka dunia izuie ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya Iran
Mar 15, 2020 23:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewaandikia barua mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa nchi mbali mbali duniani, akiwaomba wazuie na kukomesha ugaidi wa kiuchumi wa Marekani dhidi ya taifa hili.
-
Zarif asisitiza udharura wa kuondolewa vikwazo vyote haramu vya Marekani dhidi ya Iran
Mar 12, 2020 11:58Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif, amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisisitiza ulazima wa kuondolewa vikwazo haramu vya upande mmoja ilivyoekewa Iran na Marekani.
-
Zarif: Ugaidi wa kiuchumi wa Marekani umegeuka na kuwa ugaidi wa kimatibabu
Mar 07, 2020 23:15Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Rais Donald Trump ameshadidisha vikwazo haramu vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran kwa lengo la kufyonza rasilimali za taifa hili zinazohitajika kwa ajili ya kupambana na virusi hatari vya Corona.
-
"Njia sahihi ya kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, ni Ulaya kufungamana na JCPOA"
Feb 16, 2020 04:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran inataraji kuwa nchi za Ulaya zitafungamana na ahadi zake kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama zilizovyoahidi, na kwamba hatua hiyo ndiyo njia pekee na sahihi ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yaliyopo.
-
"Ni fedheha kwa Marekani kuwaunga mkono Wairani wanaofanya fujo"
Nov 19, 2019 04:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ni fedheha kwa Marekani kutangaza wazi wazi kuwa inawaunga mkono wanaofanya fujo na kuzusha ghasia kwa kisingizio cha kulalamikia ongezeko la bei ya petroli hapa nchini.
-
Zarif: EU haijachukua hatua yoyote ya maana ya kulinda JCPOA
Nov 12, 2019 04:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezikosoa nchi za Ulaya kwa kuakhirisha ahadi zao na kufeli kufungamana na mapatano ya nyuklia ya JCPOA, huku zikiitaka Tehran ifungamane kikamilifu na makubaliano hayo.
-
Zarif: Nchi za Ulaya zifungamane na mapatano ya JCPOA
Nov 05, 2019 23:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri wa Kiislamu ya Iran amezitaka nchi za Ulaya zifungamane na ahadi zao katika mapatano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) .
-
Iran yakosoa ukatili wa Marekani wa kumzuia Zarif kumtembelea balozi hospitalini
Sep 28, 2019 07:41Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amekosoa vikali kitendo cha kikatili cha Marekani cha kumzuia Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kumtembelea Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ambaye amelazwa hospitalini mjini New York.
-
Zarif: Vikwazo vya Marekani vinawalenga wananchi wa kawaida wa Iran
Sep 19, 2019 09:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali hatua ya utawala wa Rais Donald Trump wa Marekani ya kutangaza vikwazo vipya dhidi ya taifa hili na kusisitiza kuwa, kushadidishwa ugaidi huo wa kiuchumi kwa mara nyingine kumeonesha namna Washington inavyowalenga Wairani wa kawaida.
-
Zarif: Israel, mwana kilizi, ndiye mmiliki halisi wa silaha za nyuklia
Sep 10, 2019 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu matamshi ya kijuba ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, aliyedai kuwa ana ushahidi mpya unaoonesha kuwa Tehran inaunda kwa siri silaha za nyuklia; ambapo amesema kauli hiyo ya kichochezi ya Benjamin Netanyahu inalenga kufanikisha ajenda ya vita ya utawala huo haramu.