Mar 08, 2020 02:45 UTC
  • Zarif: Ugaidi wa kiuchumi wa Marekani umegeuka na kuwa ugaidi wa kimatibabu

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Rais Donald Trump ameshadidisha vikwazo haramu vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran kwa lengo la kufyonza rasilimali za taifa hili zinazohitajika kwa ajili ya kupambana na virusi hatari vya Corona.

Katika ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Dakta Zarif amesema, Trump ameshadidisha vikwazo hivyo vya kidhalimu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika hali ambayo wananchi wa Iran wanapoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Ameeleza bayana kuwa, "dunia haipaswi kuendelea kunyamazia kimya ugaidi wa kiuchumi wa Marekani ambao sasa umegeuka na kuwa ugaidi wa kimatibabu."

Jana Jumamosi, Kianoush Jahanpour, Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari cha Wizara ya Afya ya Iran alisema watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Iran kufikia jana ilikuwa ni 5,823, kati ya hao 145 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo lakini waliopona ni watu zaidi ya 1,600. 

Wahudumu wa afya wa Iran katika jitihada za kupambana na Corona

Katika hali ambayo Washington mnamo Februari 28 ilichukua hatua ya kinafiki na kimaonyesho na kutangaza kuwa itaruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Iran kupitia Uswisi, lakini aghalabu ya mashirika ya kigeni yamesita kutumia fursa hiyo yakihofia 'kuadhibiwa' na Marekani baadaye.

Ugaidi huo wa kiuchumi wa Marekani umesababisha mchakato wa kuingiza hata bidhaa muhimu za matibabu hapa nchini kuwa mgumu.

Tags