-
Yukiya Amano: Iran imefungamana kikamilifu na makubaliano ya nyuklia
May 09, 2018 09:40Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwa mara nyingine tena amethibitisha kwamba, Iran imeheshimu na kufungamana kikamilifu na makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
-
Kiongozi: Msiziamini nchi 3 za Ulaya katika mapatano ya JCPOA
May 09, 2018 09:34Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria baadhi ya matamshi kuhusu Iran kuendelea kuwepo katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA na nchi tatu za Ulaya na kusisitiza kuwa: "Kuhusu kufanya mazungumzo na nchi tatu za Ulaya, haipaswi kuziamiani na katika kila mapatano lazima kuwepo dhamana ya kweli na ya kivitendo la sivyo haiwezekani kuendelea kwa hali iliyopo."
-
Bunge la Iran lalaani hatua ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya JCPOA
May 09, 2018 09:22Wabunge katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, wameitaka serikali ya Iran itekeleza Kipengee cha 3 cha Sheria ya Hatua Mkabala Kuhusuaiana na Utekelezwaji Mapatano ya Nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA).
-
Kujitoa katika JCPOA au kujenga uadui na Jamii ya Kimataifa
May 09, 2018 08:38Hatimaye Marekani imejitoa kwenye makubaliano ya pamoja ya nchi saba ukiwemo Umoja wa Ulaya, ambayo utekelezaji wake ulidhaminiwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Walimwengu wajibu ujuba wa Marekani wa kujitoa katika JCPOA, Israel na Saudia zamuunga mkono Trump
May 09, 2018 03:27Umoja wa Ulaya, viongozi mbalimbali wa nchi za Ulaya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na wengine wengi wametoa majibu makali dhidi ya hatua ya kijuba ya rais wa Marekani ya kupuuza maamuzi ya walimwengu na ya Umoja wa Mataifa na kutangaza kujitoa katika mapatano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la JCPOA.
-
Bloomberg: Mashirika ya Boeing na Airbus ya Marekani yapata hasara kubwa kwa kujitoa Trump katika JCPOA
May 09, 2018 03:21Mashirika mawili makubwa ya kutengeneza ndege ya Boeing na Airbus ya nchini Marekani yatapata hasara kubwa ya dola bilioni 40 baada ya rais wa nchi hiyo Donald Trump kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Shamkhani: Kuvunjika makubaliano ya JCPOA hakutainufaisha Marekani
May 08, 2018 12:33Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza kuwa kuvunjika kwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hakutakuwa na manufaa kwa Marekani; na akatoa indhari pia kwa mwenendo wa nchi za Ulaya wa kutaka kujipatia fursa zaidi kwa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Wamarekani wengi wanataka US ibakie kwenye JCPOA
May 08, 2018 12:28Utafiti wa maoni wa hivi punde unaonyesha kuwa thuluthi mbili ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa nchi yao haipaswi kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran, huku yakiwa yamesalia masaa machache kabla Rais Donald Trump atangaze iwapo Washington itajiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa au la.
-
Troika ya Ulaya: Tutalinda makubaliano ya JCPOA bila kujali uamuzi wa Trump
May 07, 2018 20:54Nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zimetoa taarifa ya pamoja na kuutangazia ulimwengu kuwa zitaendelea kuheshimu mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila ya kujali uamuzi wa Marekani.
-
Qassemi: Iwapo Marekani itajitoa katika JCPOA, itapata pigo kubwa
May 07, 2018 10:59Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, iwapo Marekani itajitoa katika mapatano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA, basi madhara yake yataikumba Washington yenyewe kabla ya upande mwingine wowote.