-
Baraza la Usalama la UN lathibitisha Iran imetekeleza makubaliano ya JCPOA
Jan 19, 2017 01:10Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetangaza katika kikao chake kilichofanyika usiku wa kuamkia leo kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza majukumu yake yote kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya Tehran na kundi la 5+1 maarufu kwa kifupi kama JCPOA.
-
Iran: Iwapo Trump ataachana na JCPOA atashangazwa mwenyewe
Jan 18, 2017 13:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, iwapo rais mteule wa Marekani ataamua kuachana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, hatua hiyo itamduwaza na kumuweka kinywa wazi yeye mwenyewe.
-
Amano: Iran imeheshimu kikamilifu makubaliano ya nyuklia
Jan 18, 2017 00:40Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameeleza kuwa Iran imetekeleza majukumu yake yote yanayohusiana na makubaliano ya nyuklia kati yake na kundi la 5+1. i.
-
EU yasisitiza tena kutekelezwa kikamilifu JCPOA
Jan 16, 2017 11:07Umoja wa Ulaya umetilia mkazo kutekelezwa kikamilifu Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kufungamana na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya kundi la 5+1 na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Araqchi: Marekani na baadhi ya nchi zimekuwa zikikwamisha utekelezwaji wa JCPOA
Jan 15, 2017 11:02Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Tehran imekuwa ikikabiliwa na ukiukwaji wa ahadi, kigugumizi, siasa za ucheleweshaji mambo na chuki za Marekani na baadhi ya nchi katika utekelezwaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
-
Takhte-Ravanchi: Iran haitoruhusu kuangaliwa upya JCPOA
Jan 14, 2017 00:26Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya Ulaya na Marekani amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitatoa mwanya wa kuchunguzwa upya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
-
Matamshi ya Ujuba ya Waziri Mambo ya Nje wa Trump kuhusu Iran na JCPOA
Jan 12, 2017 01:23Rex Tillerson ambaye ni chaguo la Donald Trump rais mteule wa Marekani kuchukua Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo amesema iwapo ataidhinishwa kuchukua wadhifa huo, basi atapendekeza kuangaliwa upya mapatano ya nyuklia ya Iran.
-
Kamisheni ya pamoja ya JCPOA yachunguza ukiukaji ahadi wa Marekani
Jan 11, 2017 03:39Kikao cha kamisheni ya pamoja ya Iran na kundi la 5+1 katika kiwango cha Manaibu Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni kilichoitishwa kwa takwa la Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu kwa ajili ya kujadili ukiukaji wa makubaliano hayo uliofanywa na Marekani kimemalizika huko Vienna Austria kwa kutolewa taarifa.
-
Iran yataka ifidiwe baada ya Marekani kukiuka mapatano ya nyuklia
Jan 11, 2017 00:38Afisa wa ngazi za juu nchini Iran amesema hatua ya Bunge la Kongresi la Marekani kuongeza kwa muda wa miaka mingine kumi Sheria ya Vikwazo Dhidi ya Iran (ISA) ni ukiukaji wa mapatano ya nyuklia ya mwaka 2015 na kwa msingi huo Tehran inapasa ifidiwe kutokana na ukiukaji huo.
-
Salehi: Iran haitavunja makubaliano ya JCPOA
Dec 18, 2016 11:47Mkuu wa Taasisi ya Atomiki ya Iran amesema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitovunja makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina la JCPOA ila pale upande wa pili wa makubaliano hayo utakapofanya hivyo.