Kamisheni ya pamoja ya JCPOA yachunguza ukiukaji ahadi wa Marekani
(last modified Wed, 11 Jan 2017 07:09:37 GMT )
Jan 11, 2017 07:09 UTC
  • Kamisheni ya pamoja ya JCPOA yachunguza ukiukaji ahadi wa Marekani

Kikao cha kamisheni ya pamoja ya Iran na kundi la 5+1 katika kiwango cha Manaibu Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni kilichoitishwa kwa takwa la Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu kwa ajili ya kujadili ukiukaji wa makubaliano hayo uliofanywa na Marekani kimemalizika huko Vienna Austria kwa kutolewa taarifa.

Kikao hicho cha kamisheni ya pamoja ya kuratibu utekelezaji wa mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA) baina ya Iran na madola sita makubwa duniani ya kundi la 5+1 kimefanyika kwa mara ya pili kwa takwa la Iran.

Sayyid Abbas Araqchi, Mkuu wa Timu ya Iran katika kamisheni ya pamoja ya JCPOA amewaambia waandishi wa habari mjini Vienna kwamba, hatua ya Bunge la Kongresi la Marekani kuongeza kwa muda wa miaka mingine kumi Sheria ya Vikwazo Dhidi ya Iran (ISA) ni ukiukaji wa wazi wa mapatano ya nyuklia ya mwaka 2015. 

Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

Wawakilishi wa nchi wanachama katika kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezwaji (JCPOA)  nazo zimeeleza katika mkutano wao Vienna kwamba, wasiwasi wa Iran ni jaddi na  zimeitaka Marekani ichukue hatua za kuifanya Sheria ya Vikwazo Dhidi ya Iran (ISA) kutokuwa na athari na kuwekwa wazi mambo katika uwanja huo.

Wakati huo huo, Abbas Araqchi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran jana alikutana na kufanya mazungumzo mjini Vienna na Yukiya Amano, Mkurugezni Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na ambapo sambamba na kuashiria utekelezaji ahadi wa Iran kwa mujibu wa makubalino ya nyuklia, ameitaka IAEA kuendelea kuwa na nafasi chanya katika utekelezwaji wa makubaliano hayo ya nyuklia.

Tags