Amano: Iran imeheshimu kikamilifu makubaliano ya nyuklia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i23776-amano_iran_imeheshimu_kikamilifu_makubaliano_ya_nyuklia
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameeleza kuwa Iran imetekeleza majukumu yake yote yanayohusiana na makubaliano ya nyuklia kati yake na kundi la 5+1. i.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jan 18, 2017 00:40 UTC
  • Amano: Iran imeheshimu kikamilifu makubaliano ya nyuklia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ameeleza kuwa Iran imetekeleza majukumu yake yote yanayohusiana na makubaliano ya nyuklia kati yake na kundi la 5+1. i.

Yukia Amano ambaye alikuwa akihutubia kikao cha Ofisi ya Uratibu ya Baraza la Academia ya Umoja wa Mataifa (ACUNS) mjini Vienna amesema ripoti zake za mara kwa mara kwa Baraza la Magavana wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia katika mwaka uliopita zimeonesha kuwa, Iran imetekeleza majukumu yake yote katika uwanja huo.

Amano pia juzi tarehe 16 Januari sambamba na kutimia mwaka mmoja tangu makubaliano ya nyuklia ya Iran yatiwe saini kama mapatano muhimu ya kimataifa, alitoa taarifa akisema kuwa, Iran imefunga mashinepewa na miondombinu ya ziada katika taasisi zake za nyuklia katika wakati uliokuwa umeainishwa.

Nchi zilizotia saini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA

Wakati huo huo viongozi wa nchi za Ulaya wamepinga matamshi yasiyopimwa yaliyotolewa na rais mteule wa Marekani, Donald Trump kuhusu makubakiano ya nyuklia ya JCPOA kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1 na kutangaza kuwa, makubaliano hayo ya kimataifa yanapaswa kuheshimiwa.