-
Sisitizo juu ya ulazima wa kuundwa haraka iwezekanavyo serikali ya umoja wa kitaifa Libya
Mar 03, 2016 09:42Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Libya amesisitiza juu ya ulazima wa kuundwa haraka serikali ya umoja wa kitaifa huko Libya.
-
UN: Watu 28 wameuawa Libya mwaka huu 2016
Mar 02, 2016 10:47Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, watu 28 wamepoteza maisha na wengine 38 kujeruhiwa kwenye mapigano na ghasia katika maeneo mbalimbali ya Libya.
-
UN: Kuna ushahidi wa jinai za kivita Libya
Feb 26, 2016 12:46Umoja wa Mataifa umesema wahusika wote katika mgogoro wa Libya wametenda jina za kivita pamoja na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
-
Ufaransa yajipenyeza zaidi kijeshi nchini Libya
Feb 25, 2016 04:34Waziri Mkuu wa serikali isiyotambuliwa kimataifa nchini Libya amesema kuwa, kumekuweko ongezeko la wanajeshi maalumu wa Ufaransa katika miezi ya hivi karibuni nchini humo.
-
Vikosi maalum vya Ufaransa vyaingia Benghazi, Libya
Feb 24, 2016 04:08Vikosi maalumu vya Ufaransa vimewasili Benghazi, Libya kumuunga mkono Brigedia Jenerali Khalifa Haftar.
-
Libya yatahadharishwa kuhusu mashambulizi zaidi ya Daesh
Feb 23, 2016 00:08Mkuu wa Shirika la Mafuta la Taifa nchini Libya ametahadharisha kwamba, kuna uwezekano kundi la kigaidi la Daesh likafanya mashambulizi zaidi dhidi ya taasisi na vituo vya mafuta nchini humo maadamu hakujaundwa serikali ya umoja wa kitaifa.
-
Algeria: Uingiliaji kijeshi Libya unapasa uwe katika fremu ya sheria za kimataifa
Feb 21, 2016 22:09Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria amesema kuwa uingiliaji wowote wa kijeshi na oparesheni dhidi ya magaidi huko Libya unapasa kutekelezwa katika fremu ya sheria za kimataifa.
-
Kuongezeka maafa ya vita nchini Libya
Feb 21, 2016 03:23Vifo vinavyotokana na mapigano ya wapiganaji wanaojiita Baraza la Kimapinduzi la Benghazi na vikosi maalumu vya Libya vimefikia watu 14.
-
40 wauawa Libya katika hujuma ya ndege ya Marekani
Feb 19, 2016 10:05Mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na ndege ya kivita ya Marekani yamesababisha mauaji ya watu zaidi ya 40 katika mji wa Sabratha, kaskazini magharibi mwa Libya.
-
Kuakhirishwa tena zoezi la Bunge la Libya la kulipigia kura ya kuwa na imani baraza jipya la mawaziri
Feb 18, 2016 01:55Kikao cha Wabunge wa Libya cha kulipigia kura ya kuwa na imani baraza jipya la mawaziri la serikali ya umoja wa kitaifa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika limeakhirishwa tena. Wabunge 118 walihudhuria kikao cha juzi kwa ajili ya zoezi hilo ambalo limeakhirishwa na sasa litafanyika Jumanne ya wiki ijayo.