Ufaransa yajipenyeza zaidi kijeshi nchini Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1912-ufaransa_yajipenyeza_zaidi_kijeshi_nchini_libya
Waziri Mkuu wa serikali isiyotambuliwa kimataifa nchini Libya amesema kuwa, kumekuweko ongezeko la wanajeshi maalumu wa Ufaransa katika miezi ya hivi karibuni nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 25, 2016 04:34 UTC
  • Ufaransa yajipenyeza zaidi kijeshi nchini Libya

Waziri Mkuu wa serikali isiyotambuliwa kimataifa nchini Libya amesema kuwa, kumekuweko ongezeko la wanajeshi maalumu wa Ufaransa katika miezi ya hivi karibuni nchini humo.

Khalifa al-Gwell amesema makomandoo wa Ufaransa ndio wanaoonekana kuongoza vita katika mji wa Benghazi ulioko kaskazini Mashariki mwa Libya. Waziri Mkuu huyo wa serikali isiyotambuliwa rasmi kimataifa na ambayo inadhibiti mji mkuu, Tripoli amesema kuwa, kuongezeka uwepo wa kijeshi wa Ufaransa kunatia wasiwasi na ametaka Paris kuondoa mara moja wanajeshi wake katika ardhi ya Libya.

Serikali ya Waziri Mkuu, Khalifa Ghweil imelaani mashambulizi yanayofanywa na serikali halali ya Libya dhidi ya makundi yenye mfungamano na serikali ya Tripoli.

Libya ina serikali mbili na mabunge mawili lakini ni serikali moja tu na bunge moja tu ndizo zinazotambuliwa rasmi kimataifa. Taasisi hizo zimepiga kambi katika mji wa Tobrouk, mashariki mwa Libya baada ya kutimuliwa kutoka Tripoli na serikali pamoja na bunge ambazo hazitambuliwi rasmi kimataifa.