-
Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa Libya yapinga kikao cha Arab League
Jun 20, 2020 07:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa ya Libya amesema kuwa, Tripoli inapinga kufanyika kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusu masuala ya nchi hiyo.
-
HRW yataka uchunguzi kuhusu jinai za Jenerali Haftar nchini Libya
Jun 16, 2020 22:22Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetaka kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na wanamgambo wa jenerali muasi Khalifa Haftar nchini Libya.
-
Juhudi za Uturuki za kuweko kijeshi katika nchi ya Libya
Jun 14, 2020 08:08Baada ya Uturuki kuwa na uingiliaji wa kijeshi katika masuala ya ndani ya Libya na kushiriki pakubwa katika vita vya niaba, sasa viongozi wa Ankara wanazungumzi suala la kuanzisha vituo viwili vya kijeshi katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Umoja wa Mataifa wataka uchunguzi ufanyike kuhusu makaburi ya umati Libya
Jun 14, 2020 02:59Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kushtushwa kwake kutokana na kugundulika kwa makaburi ya umati nchini Libya katika siku za hivi karibuni, katika eneo ambalo hivi karibuni lilikuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo wanaojiita Libyan National Army (LNA) ambao wanaoongozwa na jenerali muasi Khalifa Haftar.
-
Mufti wa Libya atoa fatwa ya kuharamisha bidhaa za Misri, UAE na Jordan
Jun 13, 2020 02:53Mufti wa Libya ametoa fatwa ya kuharamisha ununuzi wa bidhaa kutoka Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Jordan.
-
Independent: Wafanyabiashara wa Kimagharibi wamemtapeli Haftar mamilioni ya dola
Jun 11, 2020 22:07Gazeti la Independent linalochapishwa nchini Uingereza limefuchua kwamba mamluki wa nchi za kigeni na wafanyabiashara wa nchi za Magharibi wakiwemo Waingereza, wamemtapeli jenerali muasi Khalifa Haftar mamilioni ya dola za Kimarekani.
-
17 wauawa na kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu Tripoli, Libya
Jun 11, 2020 03:27Kwa akali watu saba wameuawa na wengine zaidi ya kumi wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli.
-
Gazeti la Qatar: Kumefikiwa makubaliano ya kimataifa ya kummaliza Khalifa Haftar wa Libya
Jun 10, 2020 21:55Gazeti la al Arabi al Jadid limeripoti habari ya kufikiwa makubliano ya kimataifa ya kummaliza kabisa kisiasa jenerali muasi Khalifa Haftar wa Libya.
-
Umoja wa Afrika wazitaka pande hasimu Libya kuzingatia sheria za kimataifa
Jun 10, 2020 07:39Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amezitaka pande zinazopigana nchini Libya zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa, hasa kuhakikisha usalama wa hospitali na shule, na kuwezesha utoaji wa misaada.
-
UN yasisitiza ulazima wa kutatuliwa mgogoro wa Libya kwa njia za amani
Jun 09, 2020 03:04Uingiliaji kati wa nchi za kigeni katika mgogoro wa Libya umezidisha wasiwasi wa kimataifa kuhusu mgogoro huo. Katika mkondo huo Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake kuhusiana na hali ya Libya na umezitaka pande zote zinazohusika kuheshimu njia za kisiasa za kutatua mgogoro huo.