Umoja wa Afrika wazitaka pande hasimu Libya kuzingatia sheria za kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i61520-umoja_wa_afrika_wazitaka_pande_hasimu_libya_kuzingatia_sheria_za_kimataifa
Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amezitaka pande zinazopigana nchini Libya zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa, hasa kuhakikisha usalama wa hospitali na shule, na kuwezesha utoaji wa misaada.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 10, 2020 12:09 UTC
  • Umoja wa Afrika wazitaka pande hasimu Libya kuzingatia sheria za kimataifa

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amezitaka pande zinazopigana nchini Libya zifuate sheria ya kibinadamu ya kimataifa, hasa kuhakikisha usalama wa hospitali na shule, na kuwezesha utoaji wa misaada.

Mahamat amesema anaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya mambo nchini Libya na anasikitishwa na chaguo la kijeshi la utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo huku akisisitiza kuwa, mkondo huo utapelekea Walibya kukumbwa na masaibu na kuharibiwa miundo msingi ya nchi hiyo.

Mahamat amesisitiza wito wake wa tarehe 27 mwezi Machi kwa pande hasimu nchini Libya kuhusu kusitisha mapambano mara moja na kufanya mazungumzo chini ya utaratibu wa Taarifa ya Berlin.

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat

Amesema Umoja wa Afrika uko tayari kusaidia kutekeleza makubaliano ya usitishaji mapigano na kutoa mchango kwa ajili ya kuweka mazingira ya lazima kwa wadau wa Libya kurudi kwenye mazungumzo.

Aidha ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza maazimio ya vikwazo vya silaha kuhusu Libya.