-
Fayez al Sarraj azungumza na Kansela wa Ujerumani kuhusu mgogoro wa Libya
May 08, 2019 23:45Rais wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amezungumza na Kansela wa Ujerumaini kuhusiana na hasara zinazosababishwa na mashambulizi ya Jenerali Khalifa Haftar katika mji mkuu wa Libya, Tripoli.
-
UN: Yumkini Imarati imehusika katika mashambulizi ya Libya
May 07, 2019 03:26Jopo la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa linatathmini mashambulizi ya makombora dhidi ya mji mkuu wa Libya, Tripoli, sanjari na kuchunguza uwezekano wa kutumika ndege zisizo na rubani 'drone' za Umoja wa Falme za Kiarabu katika hujuma hizo.
-
UN yatoa mwito wa kusitishwa mapigano kwa muda nchini Libya
May 06, 2019 06:40Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL kimezitaka pande husika kusitisha mapigano kwa muda wa wiki moja kuanzia leo Jumatatu, katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Karibu watu 400 wauawa katika mapigano nchini Libya
May 04, 2019 03:44Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa, karibu watu 400 wameshauawa katika mapigano nchini Libya.
-
Kuendelea vita nchini Libya; kuzidi kuwa mbaya hali ya mambo katika mji mkuu Tripoli
Apr 30, 2019 22:01Kuendelea vita na mapigano katika mji mkuu wa Libya Tripoli kumeifanya hali ya kibinadamu katika mji huo izidi kuwa mbaya siku baada ya siku.
-
Qatar yawalaumu viongozi wa nchi za Kiarabu kwa siasa za kinafiki
Apr 29, 2019 23:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar amelaani mashambulizi yanayofanywa dhidi ya maeneo ya raia katika mji mkuu wa Libya Tripoli na kusisitiza kuwa, unafiki wa kisiasa na undumilakuwili ni mambo ambayo yameuchosha ulimwengu wa Kiarabu na ndiyo yanayochochea vitendo vya kigaidi.
-
Wasiwasi wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuharibika kwa hali ya kibinadamu Libya
Apr 29, 2019 09:28Naibu Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na kuendelea kuharibika kwa hali ya nchi hiyo na kusema kuwa huenda hali ya kibinadamu katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, ikaharibika zaidi.
-
Ndege za kivita za kigeni zimehusika katika mashambulio ya Tripoli
Apr 29, 2019 01:51Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amesema kuwa ndege za kigeni zilishiriki katika mashambulio ya hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.
-
Serikali ya Libya yaulalamikia Umoja wa Mataifa kwa kuruhusu mashambulizi ya Jenerali Haftar
Apr 28, 2019 11:42Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya imeulaumu Umoja wa Mataifa kwa kunyamazia kimya mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.
-
Watu 39,000 wakimbia makazi yao kufuatia mapigano Tripoli, Libya
Apr 27, 2019 20:44Kufuatia kushadidi mapigano katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, watu 39,000 wameripotiwa kukimbia makazi yao katika mji huo.