-
UN: Watu 56 wameuawa katika mapigano yanayoendelea Libya
Apr 11, 2019 09:28Umoja wa Mataifa umesema mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya yamesababisha watu 56 kupoteza maisha kufikia sasa.
-
Maelfu ya watu wawa wakimbizi kutokana na mapigano nchini Libya
Apr 10, 2019 20:32Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba mapigano ya hivi sasa ya nchini Libya yameshapelekea watu 4500 wa nchi hiyo kuwa wakimbizi.
-
Kongamano la 'amani na uchaguzi' Libya laakhirishwa kutokana na mapigano
Apr 10, 2019 03:16Mkutano wa kujadili mgogoro wa Libya na maandalizi ya uchaguzi ujao nchini humo uliotazamiwa kufanyika kati ya Aprili 14 na 16 magharibi mwa nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta umeakhirishwa kutokana na kushadidi mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.
-
UNICEF: Maisha ya watoto 500,000 wa Kilibya yapo hatarini
Apr 10, 2019 00:06Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umetangaza kuwa, maisha ya watoto 500,000 nchini Libya yapo hatarini kutokana na kuibuka mapigano mapya katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.
-
Magaidi wa Daesh watumia mapigano mapya Libya kuendeleza ukatili
Apr 09, 2019 21:56Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) limetumia ombwe lililosababishwa na mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya, kuanzisha wimbi jipya la mauaji nchini humo.
-
Naibu Waziri Mkuu wa Libya ajiuzulu ili kuonyesha uungaji mkono kwa Jenerali Haftar
Apr 08, 2019 11:54Naibu Waziri Mkuu wa Libya Ali al-Qatraani, amejiuzulu wadhifa wake na kuunga mkono kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, vikosi vinavyojiita Jeshi la Taifa la Libya vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.
-
Idadi ya waliouawa katika mapigano Libya yafikia watu 32
Apr 08, 2019 03:28Idadi ya watu waliouawa katika mapigano kati ya vikosi vya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa na vile vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya imeongezeka na kufikia watu 32.
-
Watu 21 wauawa katika mapigano yanayoendelea nchini Libya
Apr 08, 2019 00:01Wizara ya Afya ya Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya imetangaza kuwa, watu wasiopungua 21 wameuawa na wengine 27 kujeruhiwa kufuatia mapigano makali yanayoendelea kando kando ya mji mkuu Tripoli.
-
Waziri Mkuu wa Libya: Haftar ametusaliti kwa kuhujumu Tripoli
Apr 07, 2019 10:30Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj, anayeungwa mkono na Umoja wa Mataifa, amemtuhumu hasimu wake, Jenerali Khalifa Haftar kuwa amemsaliti kwa kuanzisha hujuma dhidi ya mji mkuu, Tripoli, jambo ambalo yamkini likaibua vita vya ndani nchini humo.
-
Duru mpya ya mgogoro wa kisiasa na kijeshi nchini Libya
Apr 06, 2019 21:47Katika hali ambayo, jamii ya kimataifa ilikuwa imeelekeza macho na masikio yake katika mkutano wa "mazungumzo ya kitaifa ya Libya" kwa ajili ya kufikia utatuzi wa kisiasa na kuvuka kipindi cha mgogoro wa sasa, mashambulio ya vikosi vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar na kusonga mbele kuelekea mji mkuu Tripoli, yameitumbukiza nchi hiyo katika kipindi kipya cha mgogoro.