-
Kaburi la umati lagunduliwa Sirte, Libya, lina zaidi ya maiti 100
Oct 14, 2018 08:56Vyombo vya usalama nchini Libya vimetangaza kuwa, vimegundua kaburi la umati lenye maiti za makumu ya watu lililoko umbali wa kilomita 15 magharibi mwa mji wa Sitre huko kakazini mwa nchi hiyo.
-
Sadiq al Kabir: Kumepatikana hasara ya dola bilioni 48 kutokana na vita vya ndani Libya
Oct 12, 2018 13:14Gavana wa Benki Kuu ya Libya amesema kuwa vita na mapigano ya ndani nchini humo husababisha hasara ya dola bilioni 48.6 kwa uchumi wa nchi hiyo kila mwaka.
-
Uchunguzi: Libya inakabiliwa na kundi jipya la Daesh
Oct 10, 2018 02:56Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa al Wasat nchini Libya umebaini kuwa, hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi hiyo inaanda mazingira ya kujitokeza kundi jipya la Daesh na kutahadharisha kuwa yumkini nchi hiyo ikawa makimbilio salama ya vinara wa makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka kutoka pembe mbalimbali za dunia.
-
Gaidi hatari zaidi wa Misri atiwa nguvuni Derna, Libya
Oct 08, 2018 23:05Msemaji wa Jeshi la Taifa la Libya ametangaza kuwa, jeshi hilo limemtia nguvuni kinara wa makundi ya kigaidi katika mkoa wa Derna huko kaskazini mwa Libya.
-
Baraza la mawaziri Libya lafanyiwa mabadiliko, mawaziri wanne wapigwa kalamu nyekundu
Oct 08, 2018 04:15Waziri Mkuu wa serikali ya maafikiano ya kitaifa ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa amelifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri kwa kuteua mawaziri wanne wapya kushika nyadhifa za Wizara ya Mambo ya Ndani, Fedha, Uchumi na Viwanda na Vijana na Michezo.
-
Ujumbe wa UN nchini Libya wapongeza utangulizi wa mipango mipya ya kiusalama
Oct 07, 2018 11:47Ujumbe wa usaidizi wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) umepongeza mipango mipya ya kiusalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli iliyobuniwa na Baraza la serikali la uongozi.
-
Libya yapinga uingiliaji wa kijeshi wa madola ajinabi nchini humo
Oct 06, 2018 11:43Mjumbe wa Baraza Kuu la Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya amepinga njama za jeshi la nchi za Magharibi NATO za kutaka kuingilia tena kijeshi nchini humo na kusema kuwa, Libya inapinga uingiliaji wowote wa kijeshi wa madola ya kigeni.
-
Serikali ya umoja wa kitaifa Libya yaunga mkono mchakato wa uchaguzi
Sep 30, 2018 10:55Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amekutaja kufanyika chaguzi za bunge na rais nchini humo kuwa njia bora zaidi kwa ajili ya kurejesha amani nchini humo.
-
Mapigano yaanza upya mjini Tripoli, Libya
Sep 29, 2018 11:54Vyombo mbalimbali vya habari vimetangaza kuwa, utulivu katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, haukudumu ila kwa siku chache tu kwani tayari mapigano yameanza upya mjini humo.
-
Mahasimu wakubaliana kusitisha vita vilivyoua 117 Tripoli, Libya
Sep 26, 2018 23:30Makundi mawili hasimu ya waasi nchini Libya yamekubaliana kusitisha mapigano yaliyopelekea kuuawa makumi ya watu katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.