Uchunguzi: Libya inakabiliwa na kundi jipya la Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48696-uchunguzi_libya_inakabiliwa_na_kundi_jipya_la_daesh
Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa al Wasat nchini Libya umebaini kuwa, hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi hiyo inaanda mazingira ya kujitokeza kundi jipya la Daesh na kutahadharisha kuwa yumkini nchi hiyo ikawa makimbilio salama ya vinara wa makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka kutoka pembe mbalimbali za dunia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 10, 2018 02:56 UTC
  • Uchunguzi: Libya inakabiliwa na kundi jipya la Daesh

Uchunguzi uliofanywa na mtandao wa al Wasat nchini Libya umebaini kuwa, hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi hiyo inaanda mazingira ya kujitokeza kundi jipya la Daesh na kutahadharisha kuwa yumkini nchi hiyo ikawa makimbilio salama ya vinara wa makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka kutoka pembe mbalimbali za dunia.

Ripoti ya mtandao huo imesema kuwa, mazingira ya sasa ya Libya yanaandaa uwanja mzuri wa kudhihiri kundi jipya la Daesh japokuwa kundi hilo limedhoofika na kupoteza uwezo wake. 

Ripoti hiyo imesisitiza kuwa, sababu nyingi ikiwa ni pamoja na machafuko ya ndani, udhaifu wa kikosi cha usalama, kuzagaa silaha baina ya wananchi na kutokuwepo serikali kuu yenye nguvu, vinachangia kutayarisha mazingira ya kudhihiri kundi jipya na hatari zaidi la Daesh nchini Libya.

Libya inasumbuliwa na machafuko ya ndani.

Al Wasat imeripoti kuwa mbegu ya kwanza ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Libya ilipandikizwa na mawahabi kutoka Saudi Arabia na kwamba hali ya sasa ya nchi hiyo inashabihiana na ile iliyokuwepo Bara Arabu wakati kundi hilo lilipoanzishwa. 

Kwa sasa Libya inaongozwa na serikali mbili hasimu, ile inayoongozwa na Fayez al-Sarraj yenye makao makuu Tripoli na nyingine ya Tobruk huko mashariki mwa Libya inayoongozwa na Abdullah al-Thani.