-
Maandamano yaendelea Sudan, wahadhiri wa vyuo vikuu watiwa nguvuni
Jan 06, 2019 09:11Askari usalama wa Sudan wamewatia nguvuni wahadhiri wa vyuo vikuuu walioanzisha mgomo leo mjini Khaertoum na kukabiliana na waandamanaji kwa mabomu ya kutoa machozi.
-
Muungano mkuu wa upinzani nchini Sudan wamtaka Rais Bashir ajiuzulu
Jan 02, 2019 23:43Muungano mkubwa zaidi wa upinzani wa Nidaa nchini Sudan umemtaka Rais Omar al-Bashir wa nchi hiyo aachie ngazi, huku maandamano dhidi ya serikali yakiendelea.
-
Umoja wa Mataifa wataka kufanyike uchunguzi kuhusu mauaji ya waandamanaji Sudan
Dec 29, 2018 12:53Umoja wa Mataifa umelezea kusikitishwa sana na machafuko pamoja na mauaji ya waandamanaji nchini Sudan na umewataka viongozi wa nchi hiyo wafanye uchunguzi unaotakiwa wa kubaini kwa nini waandamanaji wanauawa.
-
Helikopta ya Israel yawashambulia Wapalestina wa Ukanda wa Gaza
Dec 29, 2018 04:28Helikopta ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel imeshambulia maeneo ya kusini mwa Ukanda wa Gaza, kwa madai kuwa hujuma hiyo ni ya ulipizaji kisasi baada ya Wapalestina kuwavurumishia roketi.
-
Polisi Sudan wawashambulia waandamanaji wakitoka msikitini
Dec 28, 2018 12:37Maafisa usalama nchini Sudan wamewashambulia kwa mabomu ya kutoa machozi, waumini wa Kiislamu waliokuwa wakishiriki 'maandamano ya amani' baada ya Sala ya Ijumaa, katika mji wa Omdurman, nje kidogo ya mji mkuu Khartoum.
-
'Maandamano ya Mkate' yazidi kuigubika Sudan, Rais al-Bashir akalia kuti kavu
Dec 27, 2018 11:28Maandamano ya mkate ambayo yamekuwa yakishushuhudiwa nchini Sudan kwa wiki moja sasa na ambayo yamechukua mkondo wa kisiasa, yamezidi kuigubika nchi hiyo na kuifanya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir ikabiliwe na mashinikizo zaidi.
-
Rais al Bashir atishia kukata mikono ya waandamanaji Sudan
Dec 27, 2018 04:16Rais Hassan al Bashir wa Sudan amekemea vikali "maandamano ya mkate" yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini humo dhidi ya serikali yake na kusema kuwa atakata mikono ya waandamanaji hao.
-
Msudan mwingine auawa katika maandamano
Dec 26, 2018 09:52Baada ya kuuawa Msudan mwingine katika maandamano ya kupinga serikali, idadi ya wahanga waliopoteza maisha yao katika maandamano yaliyoanza wiki iliyopita, wameshafikia 38.
-
Amnesty: Watu 37 wameuawa katika 'maandamano ya mkate' Sudan
Dec 25, 2018 23:36Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema makumi ya watu wameuawa katika makabiliano baina ya polisi na waandamanaji nchini Sudan.
-
Wapinzani: Waliouawa katika 'maandamano ya mkate' Sudan ni 22
Dec 23, 2018 03:53Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Sudan, Sadiq al-Mahdi amedai kuwa watu waliouawa na maafisa usalama katika maandamano ya kulalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kama mkate na hali mbaya ya uchumi ni 22.