Rais al Bashir atishia kukata mikono ya waandamanaji Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i50452-rais_al_bashir_atishia_kukata_mikono_ya_waandamanaji_sudan
Rais Hassan al Bashir wa Sudan amekemea vikali "maandamano ya mkate" yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini humo dhidi ya serikali yake na kusema kuwa atakata mikono ya waandamanaji hao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2018 04:16 UTC
  • Rais Hassan al Bashir wa Sudan
    Rais Hassan al Bashir wa Sudan

Rais Hassan al Bashir wa Sudan amekemea vikali "maandamano ya mkate" yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini humo dhidi ya serikali yake na kusema kuwa atakata mikono ya waandamanaji hao.

Al Bashir amesema kuwa atakandamiza vikali maandamano hayo na kwamba jeshi la Sudan litaharibu maisha ya waandamanaji na kukata mikono yao.

Rais wa Sudan amesisitiza waziwazi kwamba, hatasalimu amri mbele ya matakwa ya taifa la Sudan au matakwa ya wasaliti. Vilevile amewatahadharisha Wasudani kuhusu kile alichokiita uvumi na kusema kuwa, mwenendo wa marekebisho umeshika njia yake nchini Sudan.

Matamshi hayo makali ya Rais Omar al Bashir wa Sudan yametolewa kufuatia maandamano yanayoendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo dhidi ya hali mbaya ya uchumi na ughali wa bidhaa muhimu hususan mkate ambao ndio cakula kikuu cha Wasudani.

Miji ya Sudan imekuwa uwanja wa mapambano baina ya jeshi na raia

Maandamano ya Wasudani yaliyoanza kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi yamepata sura nyingine na sasa waandamanaji wanataka kuondolewa madarakani serikali ya Omar al Bashir.

Watu wasiopungua 38 wameuawa hadi sasa katika maandamano hayo.