-
Watu watatu wafariki dunia nchini Kenya katika maandamano ya wapinzani wa serikali
May 23, 2016 23:12Watu watatu wamepoteza maisha yao na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Kenya baada ya maandamano ya mrengo wa upinzani ya kutaka Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ijiuzulu kugeuka na kuwa uwanja wa fujo.
-
Wafungwa wa Misri wasusia chakula kukosoa 'kesi bandia'
May 23, 2016 07:47Makumi ya wafungwa wa Misri walioshiriki maandamano ya kuikosoa serikali ya Cairo kwa kuipa Saudi Arabia visiwa viwili vinavyomilikiwa na nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika wanafanya mgomo wa kula, kulalamikia kile walichokitaja kuwa kesi bandia na za kidhulma dhidi yao.
-
Upinzani Kenya: Wabunge wa Jubilee wanapanga njama ya kuahirisha uchaguzi mkuu 2017
May 22, 2016 23:03Viongozi wa upinzani nchini Kenya wamedai wabunge wa muungano tawala wa Jubilee wanapanga njama ya kuvuruga maandamano yao ya amani ambayo hufanyika kila Jumatatu kwa lengo la kushinikiza kujiuzulu makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, ili itangaze hali ya hatari na hatimaye kuahirisha uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao wa 2017.
-
Wanaharakati Uingereza waandamana dhidi ya Rais wa Nigeria, wataka kuachiwa Sh. Zakzaky
May 13, 2016 03:21Makundi ya waharakati wa kutetea haki za binadamu yamefanya maandamano katika mji mkuu wa Uingereza London kulalamikia dhuluma na ukandamizaji unaofanywa na vyombo vya usalama vya Nigeria dhidi Waislamu wa nchi hiyo.
-
Wapinzani Kenya wakaidi amri na kuandamana kupinga tume ya uchaguzi
May 09, 2016 10:49Wafuasi wa muungano wa upinzani wa Cord nchini Kenya wamekaidi amri ya serikali na kuibua ghasia nje ya makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi IEBC mjini Nairobi.
-
Wapalestina waandamana Ukanda wa Gaza kulaani mzingiro wa Israel
May 08, 2016 08:37Mamia ya wananchi wa Palestina wameingia mabarabarani kufanya maandamano ya kulaani mzingiro wa kibaguzi wa takriban mwongo mmoja uliowekwa na Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Wananchi wa Bahrain waandamana kushinikiza kuachiwa Sh. Salman
Apr 30, 2016 03:28Kwa mara nyingine tena wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano katika barabara za nchi hiyo kushinikiza kuachiwa huru msomi mashuhuri wa Kiislamu Sheikh Ali Salman.
-
Polisi Uganda: Maandamano ya upinzani hayana kibali
Apr 30, 2016 03:27Polisi ya Uganda imeonya wafuasi wa upinzani nchini humo dhidi ya kushiriki maandamano ya Mei 5 na kusisitiza kuwa maandamano hayo hayajapata ridhaa ya serikali.
-
Wanaharakati: Mapambano Bahrain kuendelea hadi matakwa yatimizwe
Apr 27, 2016 23:33Kiongozi wa mrengo wa Februari 14 nchini Bahrain amelaani wimbi la ukandamizaji na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Aal-Khalifa dhidi ya wananchi na kusisitiza kuwa mapambano ya wapinzani yataendelea hadi matakwa yao yote yatakapotimizwa.
-
Maandamano ya Siku ya Wafungwa wa Kipalestina
Apr 17, 2016 23:41Mamia ya wananchi wa Palestina jana Jumapili walifanya maandamano katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Gaza katika maadhimisho ya Siku ya Wafungwa wa Kipalestina.