Wananchi wa Bahrain waandamana kushinikiza kuachiwa Sh. Salman
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i6097-wananchi_wa_bahrain_waandamana_kushinikiza_kuachiwa_sh._salman
Kwa mara nyingine tena wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano katika barabara za nchi hiyo kushinikiza kuachiwa huru msomi mashuhuri wa Kiislamu Sheikh Ali Salman.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 30, 2016 03:28 UTC
  • Wananchi wa Bahrain waandamana kushinikiza kuachiwa Sh. Salman

Kwa mara nyingine tena wananchi wa Bahrain wamefanya maandamano katika barabara za nchi hiyo kushinikiza kuachiwa huru msomi mashuhuri wa Kiislamu Sheikh Ali Salman.

Maandamano makubwa yalishuhudiwa baada ya swala ya Ijumaa katika kijiji cha Diraz, yapata kilomita 12 magharibi mwa mji mkuu Manama.

Waandamanaji hao waliokua wamebeba mabango yaliyokuwa na picha ya Sheikh Salman wameutaka utawala wa Manama kumuachia huru mara moja msomi huyo wa Kishia ambaye ni kinara wa chama kikuu cha upinzani cha al-Wifaq.

Hadi sasa maelfu ya wanaharakati na viongozi wa kidini akiwemo Sheik Ali Salman, Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Al-Wifaq, wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za utawala huo wa Bahrain mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa.

Hata hivyo na pamoja na ukandamizaji huo, maandamano dhidi ya utawala huo yameendelea kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya utawala huo kibaraka wa Saudi Arabia.