-
Araqchi: Iran imepunguza uwajibikaji wake ili kuyalinda makubaliano ya JCPOA
Nov 12, 2019 08:34Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika Masuala ya Kisiasa amesema kuwa lengo la Tehran kupunguza ahadi na uwajibikaji wake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni kwa ajili ya kuyalinda makubaliano hayo.
-
"Marekani inachochea maandamano katika nchi za Kiarabu kwa maslahi yake"
Nov 12, 2019 04:41Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, Marekani inatumia maandamano yanayoshuhidiwa hivi sasa katika nchi kadhaa za Kiarabu kusukuma ajenda zake, na kuifanya Lebanon ishindwe kujisimamia yenyewe.
-
Indhari ya Mshauri wa Usalama wa Taifa Marekani kuhusu kusambaratika NATO
Nov 12, 2019 04:27Rais Donald Trump wa Marekani ambaye ni maarufu kwa kuibua utata, angali anaendelea kukosoa vikali Muungano wa Kijeshi wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) . Trump hasa anawakosoa wanachama wa bara Ulaya katika muungano huo kwa kutotenga asilimia 2 ya Pato la Ndani la Nchi (GDP) kwa ajili ya gharama za kijeshi. Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani nao sasa pia wanafuata nyayo za Trump katika kuukosoa muungano wa kijeshi wa NATO.
-
Sisitizo la jeshi la Marekani la kuendelea kuwepo kijeshi katika eneo la Asia Magharibi
Nov 11, 2019 23:26Licha ya Rais Donald Trump kukariri mara chungu nzima kwamba, Washington itaondoa wanajeshi wake katika eneo la Asia Magharibi hususan katika nchi za Syria na Afghnaistan, lakini hali ya mambo ilivyo inaonyesha kuwa, Marekani imeazimia kubakisha na hata kuongeza idadi ya wanajeshi wake pamoja na zana za kijeshi katika eneo hili ikiwa ni katika kusukuma mbele gurudumu la siasa zake za kibabe.
-
Uturuki yamrejesha mwanachama wa ISIS nchini Marekani
Nov 11, 2019 07:54Uturuki imesema imemrejesha mwanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika nchi yake ya Marekani, huku Ankara ikianza kuwarejesha makwao magaidi wa genge hilo la ukufurishaji iliowakamata.
-
Rais Bashar Al Assad: Yumkini Marekani haijamuua Baghdadi, bali imemficha
Nov 11, 2019 07:50Rais Bashar al-Assad wa Syria ametilia shaka madai ya Marekani kuwa imemuua kinara wa kundi la kigaidi la Daesh, Abu Bakr Baghdadi, na kusisitiza kwamba huenda kiongozi huyo wa ISIS amejificha au amefichwa sehemu fulani na serikali ya Washington.
-
Rais wa Ujerumani akosoa sera za kijuba za Marekani
Nov 11, 2019 03:35Siasa za kijuba na misimamo inayokiuka sheria za kimataifa ya Marekani imekuwa ikipingwa na kukosolewa na nchi nyingi duniani na hata washirika wa nchi hiyo barani Ulaya.
-
Russia yaonya kuhusu hatari ya ISIS nchini Afghanistan na uungaji mkono wa Marekani kwa kundi hilo
Nov 10, 2019 03:50Russia imeonya mara kadhaa kuhusu kuenea harakati za kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) nchini Afghanistan na kuongeza kuwa magaidi hao wakufurishaji wanaungwa mkono na Marekani.
-
Iran: Miungano ya Marekani inasababisha machafuko kote ulimwenguni
Nov 09, 2019 10:03Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, miungano mbalimbali inayoundwa na Marekani inasababisha machafuko katika kona zote za dunia na kuhatarisha usalama na amani ya kila eneo lenye miungano hiyo.
-
Korea Kaskazini: Mazungumzo yetu na Marekani yanakaribia kuvunjika kikamilifu
Nov 09, 2019 04:32Mkuu wa kitengo cha masuala ya Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, ameelezea uwezekano wa kuvunjika kikamilifu mazungumzo kati ya Washington na Pyongyang, kutokana na ukwamishaji mambo wa Marekani.