-
Ubalozi wa Marekani Baghdad washambuliwa baada ya safari ya kinyemela ya Trump nchini Iraq
Dec 27, 2018 04:16Ubalozi wa Mrekani mjini Baghdad nchini Iraq umeshambuliwa kwa maroketi mapema leo Alkhamisi masaa machache baada ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kufanya safari ya kinyemela nchini Iraq akiandamana na mkewe.
-
Amnesty yaitaka Marekani isitishe ukatili dhidi ya wahajiri
Dec 27, 2018 03:25Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekosoa sera za kikatili za serikali ya Marekani kuhusiana na wahajiri na kutoa wito wa kubadilishwa mwenendo huo.
-
Ujerumani yapinga kuwekwa silaha za nyuklia za Marekani katika ardhi yake
Dec 27, 2018 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema kuwa Berlin inapinga suala la kuwekwa silaha za masafa ya kati za nyuklia za Marekani katika ardhi yake.
-
Mamilionea wa Marekani wasema hawataunga mkono kampeni za Trump 2020
Dec 25, 2018 10:58Utafiti wa maoni uliofanywa na shirika la habari la CNBC unaonesha kuwa Rais Donald Trump wa Marekani anaendelea kupoteza uungaji mkono sio tu miongoni mwa wananchi, bali pia miongoni mwa wafanyabiashara matajiri waliomuunga mkono katika kampeni zake za uchaguzi uliopita mwaka 2016.
-
Dakta Zarif: Tangu awali kuweko Marekani nchini Syria kulikuwa kinyume cha sheria
Dec 24, 2018 23:28Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, katu Marekani haijawahi kupambana na kundi la kigaidi la Daesh na kwamba, Washington haikuwa nchini Syria kwa faida ya wananchi wa nchi hiyo wala kwa ridhaa ya serikali ya Damascus.
-
Ayatullah Amoli Larijani: Marekani imekimbia nchini Syria
Dec 24, 2018 11:29Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria hatua ya Marekani ya kuondoa majeshi yeke Syria na kusema kuwa, Marekani imekimbia kutoka katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Shughuli za serikali ya Marekani Zaendelea kukwama, Trump hana Krismasi
Dec 24, 2018 01:08Sehemu kubwa ya shughuli za serikali ya Marekani zitaendelea kusitishwa kwa siku tano, kutokana na mkwamo kwenye ufadhili wa ujenzi wa ukuta wa kuzuia wahajiri katika mpaka wa Marekani na Mexico.
-
Mshauri wa Bashar al-Assad: Wamarekani wamekimbia Syria
Dec 23, 2018 23:20Mshauri wa kisiasa na wa masuala ya habari wa Rais wa Syria amesema kuhusu hatua ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini humo kwamba: Wamarekani wamekimbia, kwa sababu sisi tumesimama imara.
-
WikiLeaks: Balozi za Marekani duniani zimerundika vifaa vya ujasusi
Dec 23, 2018 04:41Mtandao wa WikiLeaks umefichua kuwa, balozi za Marekani na vituo vingine vyake vya kidiplomasia kote duniani vimenunua kiwango kikubwa cha vifaa na suhula za kijasusi; katika hali ambayo baadhi ya nchi zimekuwa zikieleza hofu yao kwamba balozi hizo za Marekani badala ya kujihusisha na masuala ya udiplomasia pamoja na uhusiano mwema, zinahusika zaidi na masuala ya ujasusi, mapinduzi ya serikali halali na njama zinginezo haribifu kote duniani.
-
Hizbullah Iraq: Kuondoka Marekani syria ni ishara ya kushindwa Washington
Dec 22, 2018 21:39Harakati ya Hizbullah ya Iraq imetangaza kuwa, kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini Syria kuna maana ya kushindwa stratijia za jeshi la nchi hiyo.