-
Wabunge wa Uganda watuma faili la mauaji ya Kasese ICC
Jan 05, 2017 12:40Kundi la wabunge wa Uganda limetuma ombi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, likiitaka ianzishe uchunguzi juu ya mauaji yanayodaiwa kufanywa na maafisa usalama katika mji wa Kasese, jimbo la Rwenzori mwishoni mwa mwaka uliopita 2016.
-
HRW: Serikali inaficha jinai na mauaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar
Jan 05, 2017 12:39Mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Human Rights Watch yamesema serikali ya Myanmar inajaribu kuficha jinai na mauaji yanayofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
-
Polisi: Waziri auawa kwa kufyatuliwa risasi Bujumbura, Burundi
Jan 01, 2017 03:49Waziri wa Mazingira wa Burundi ameuawa kwa kufyatuliwa risasi na mtu asiyejulikana usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura.
-
Hali yazidi kuwa tete DRC, 52 wauawa katika maandamano, mapigano ya kikabila
Dec 22, 2016 13:30Hali ya mambo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imezidi kuwa tete huku makumi ya watu wakiuawa katika maandamano na mapigano ya kikabila.
-
Bunge la Tunisia kuchunguza mauaji ya msomi Al Zawari wa nchi hiyo
Dec 22, 2016 11:15Bunge la Tunisia linakutana kesho Ijumaa katika kikao cha dharura kuchunguza faili la mauaji ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya msomi wa masuala ya anga wa nchi hiyo, Muhammad al Zawari.
-
Iran, UN zalaani mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki
Dec 20, 2016 04:23Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki na kuutaja ukatili huo kama kitendo cha kikatili na kishenzi.
-
Amnesty 'yashtushwa' na mauaji ya halaiki nchini Uganda
Nov 29, 2016 10:27Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani kile lilichokitaja kuwa mauaji ya halaiki katika eneo la Rwenzori, kusini magharibi mwa Uganda.
-
UN yatadharidha kutokea mauaji ya kimbari Sudan Kusini
Nov 12, 2016 04:16Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa ameonya kuwa yumkini Sudan Kusini ikatumbukia katika mauaji ya kimbari kutokana na kushadidi mapigano ya kikabila nchini humo.
-
38 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano Niger
Nov 02, 2016 11:00Watu 18 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa katika mapigano makali kati ya wakulima na wafugaji nchini Niger.
-
Ufaransa yafufua uchunguzi wa mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda
Oct 08, 2016 10:26Ufaransa imeanzisha tena uchunguzi wa mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana, yaliyopelekea kuanza kwa mauji ya kimbari nchini humo mwaka 1994.