Bunge la Tunisia kuchunguza mauaji ya msomi Al Zawari wa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21928-bunge_la_tunisia_kuchunguza_mauaji_ya_msomi_al_zawari_wa_nchi_hiyo
Bunge la Tunisia linakutana kesho Ijumaa katika kikao cha dharura kuchunguza faili la mauaji ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya msomi wa masuala ya anga wa nchi hiyo, Muhammad al Zawari.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 22, 2016 11:15 UTC
  • Bunge la Tunisia kuchunguza mauaji ya msomi Al Zawari wa nchi hiyo

Bunge la Tunisia linakutana kesho Ijumaa katika kikao cha dharura kuchunguza faili la mauaji ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya msomi wa masuala ya anga wa nchi hiyo, Muhammad al Zawari.

Mtaalamu huyo wa masuala ya anga wa Tunisia ambaye alikuwa akishirikiana na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) katika kutengeneza ndege zisizo na rubani (drones) aliuawa Alkhamisi iliyopita kwa kupigwa risasi alipokuwa katika gari lake binafsi katika mji wa Sfax ulioko kusini mwa nchi hiyo.

Wabunge wa Tunisia wamewataka Mawaziri wa Mambo na Nje na Mambo ya Ndani kuhudhuria bungeni kwa ajili ya kutoa maelezo kamili juu ya mauaji ya kigaidi ya msomi huyo.

Vyombo vya mahakama nchini Tunisia vimekamilisha uchunguzi na kuwahoji watuhumiwa 10 waliokamatwa kwa kuhusika la faili la mauaji ya Muhandisi Muhammad al Zawari na vimetuma picha ya raia mmoja wa Ubelgiji kwa polisi ya kimataifa Interpol ambaye anatuhumiwa pia kuhusika na mauaji hayo.

Muhammad al Zawari

Mauaji ya msomi huyo wa Tunisia yamezusha utata mkubwa na kuna uwezekano  kwamba shirika la ujasusi la Israel Mossad ndilo lililopanga jinai hiyo na kigaidi.

Miaka 8 iliyopita pia shirika la ujasusi la Israel, Mossad lilimuua kigaidi Khalil al Wazir maarufu kwa jina la Abu Jihad ambaye alikuwa kamanda wa harakati ya Palestina ya Fat'h akiwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Sidi Bousaid kaskazini mwa mji mkuu wa Tunisia, Tunis.