-
Jinai mpya ya Boko Haram, muendelezo wa misimamo ya kufurutu ada Afrika
Nov 30, 2020 09:44Baada ya makundi ya kigaidi kudhoofishwa katika maeneo mbali mbali ya Asia Magharibi, hivi sasa makundi hayo yameeneza satwa yao na kuimarika katika maeneo mbali ya barani Afrika ambapo yamekithirisha hujuma. Katika tukio la hivi karibuni, magaidi wakufurishaji wa Boko Haram wameua wakulima 110 katika kijiji cha Koshobe karibu na Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno ambalo ni kitovu cha magaidi hao, kaskazini mashariki mwa Nigeria.
-
Kuendelea malalamiko ya Wanigeria katika kumtetea Sheikh Zakzaki
Nov 26, 2020 06:14Katika kuendelea kushikiliwa kinyume cha sheria Sheikh Ibrahim Zakzaki, Kiongozi wa Waislamu wa Nigeria, Waislamu wa nchi hiyo kwa mara nyingine tena wamefanya maandamano makubwa ya kuunga mkono na kutaka mwanzuoni huyo wa Kiislamu aachiliwe mara moja.
-
Boko Haram yatungua helikopta Nigeria na kuua watu 5
Nov 19, 2020 03:25Kundi la kigaidi la Boko Haram limetungua ndege aina ya helikopta huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuua watu watano.
-
Wananchi wa Nigeria watoa ushahidi kuhusu jinai za jeshi la nchi hiyo
Nov 15, 2020 23:05Kamati ya Mahakama ya Nigeria imeripoti kuwa, raia wa nchi hiyo wamewasilisha ushahidi wao wa kimaandishi kuhusu jinai na uhalifu uliofanywa na jeshi la nchi hiyo dhidi ya raia.
-
Wanigeria waandamana tena kushinikiza kuachiwa huru Sheikh Zakzaky
Nov 10, 2020 03:55Wafuasi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wameandamana katika mji mkuu Abuja wakilalamikia kuendelea kushikiliwa kizuizini kiongozi wao pamoja na mkewe.
-
Wanachama 75 wa Boko Haram waangamizwa na jeshi la Nigeria
Nov 04, 2020 08:17Jeshi la Nigeria limetangaza habari ya kuuawa makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Umoja wa Afrika wataka Nigeria ichukue hatua za kusitisha ghasia, mauaji
Oct 27, 2020 08:04Umoja wa Afrika umeihimiza serikali ya Nigeria ichukue mara moja hatua za amani za mazungumzo ili kupunguza mvutano unaozidi kupamba moto nchini humo, kufanya uchunguzi kuhusu mauaji na kuwafikisha wahusika mahakamani.
-
Raia 51, maafisa usalama 18 wameuawa katika maandamano ya ghasia Nigeria
Oct 24, 2020 04:11Makumi ya watu wameuawa katika machafuko na maandamano yanayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya Nigeria.
-
Buhari ataka kukomeshwa maandamano, machafuko yaendelea Abuja
Oct 23, 2020 06:58Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametoa wito wa kukomesha machafuko na maandamano yanayoendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kufuatia mauaji ya raia waliokuwa wakiandamana kupinga ukatili wa polisi.
-
Umoja wa Afrika walaani mauaji ya raia nchini Nigeria
Oct 22, 2020 10:18Nchi ya Nigeria inaendelea kukumbwa na hali ya machafuko baada ya askari usalama kuwatawanya kikatili vijana walioandamana dhidi ya ghasia za polisi, na kuua watu kadhaa. hayo yametangaza na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.