"Saudia imeipa serikali ya Nigeria mamilioni ya dola imuue Sheikh Zakzaky"
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i65243-saudia_imeipa_serikali_ya_nigeria_mamilioni_ya_dola_imuue_sheikh_zakzaky
Wakili wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia umeipa serikali ya Abuja mamilioni ya dola ili imuue mwanaharakati huyo wa Kiislamu anayeshikiliwa kizuizini mwa miaka mitano sasa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 17, 2020 07:39 UTC

Wakili wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema utawala wa Aal-Saud wa Saudi Arabia umeipa serikali ya Abuja mamilioni ya dola ili imuue mwanaharakati huyo wa Kiislamu anayeshikiliwa kizuizini mwa miaka mitano sasa.

Shirika la habari la Tasnim limemnukuu Ishaq Adam Ishaq, wakili wa Sheikh Zakzaky akisema kuwa, serikali ya Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria imekabidhiwa mamilioni ya dola na tawala za Saudia, Marekani na Israel ili imtokomeze Sheikh Zakzaky.

Ameongeza kuwa, hali ya kiafya ya kiongozi huyo wa Kiislamu inazidi kuwa mbaya, na kwamba hivi sasa hamna yeyote mwenye taarifa mpya kumhusu kwa kuwa anazuiliwa kusikojulikana tangu mahakama moja ya nchi hiyo imuachie huru.

Hii ni katika hali ambayo, katika miezi ya karibuni wananchi wa Nigeria wamekuwa wakifanya maandamano katika miji tofauti ya nchi hiyo wakitaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru, lakini kila mara maandamano yanapofanyika askari usalama wa nchi hiyo wanatumia nguvu ya ziada kuyavunja.

Maandamano ya kushinikiza Sheikh Zakzaky na mkewe waachie huru

Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mke wake Malama Zeenat walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015  katika shambulio la uvamizi lililofanywa na askari wa jeshi la Nigeria katika Hussainiya ya Baqiyyatullah iliyoko kwenye mji wa Zaria.

Siku Sheikh Zakzaky alipotiwa nguvuni, jeshi la Nigeria liliwafyatulia risasi watu waliokuwa wamekusanyika mbele ya Hussainiya na nyumba ya Zakzaky na kuua shahidi mamia miongoni mwao wakiwemo watoto wake watatu.