Dec 16, 2020 08:11 UTC
  • Jeshi la Nigeria limefanikiwa kuwakomboa wanafunzi kadhaa waliokuwa wametekwa nyara  huko Katsina

Maafisa wa Nigeria wameeleza kuwa, wanafunzi kadhaa waliokuwa wametekwa nyara na magaidi wa kundi la Boko Haram wamekombolewa.

Aminu Masari Gavana wa jimbo la Katsina ametangaza kuwa, wanafunzi wapatao 17 wameweza kukombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Boko Haram kufuatia oparesheni iliyofanywa na jeshi la nchi hiyo. Duru za serikali ya Nigeria zimesisitiza kuwa wanafunzi wawili wamepoteza maisha katika oparesheni hiyo. Aminu Masari wakati huo huo amesisitiza kuwa yeye ndio aliyeagiza kutekelezwa oparesheni hiyo ya kuwakomboa wanafunzi waliotekwa nyara na Boko Haram. 

Masari ameongeza kuwa, akthari ya wanafunzi waliotekwa nyara ambao walikuwa wa shule moja ya sekondari katika kijiji cha Kankara katika jimbo la Katsina hivi sasa wanashikiliwa katika misitu ya Zamfara kandokando ya Katsina. 

Wakati huo huo Bashir Salihi Magashi Waziri wa Ulinzi wa Nigeria amefanya ziara huko Katsina kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuahidi kuwakomboa haraka wanafunzi hao wanaoshikiliwa na magaidi wa Boko Haram. Itakumbukwa kuwa, Ijumaa iliyopita sasa 3 na dakika 41 kwa wakati wa Nigeria watu wenye silaha waliivamia shule ya sekondari ya serikali ya  katika kijiji cha Kankara na kisha kuwateka nyara wanafunzi kadhaa wa shule hiyo ya upili ya wavulana.  

Wazazi wakatika hali ya taharuki baada ya kutekwanyara wanafunzi na Boko Haram 

 

Tags