-
Iran: Israel haijawahi kutengwa kiasi hiki katika historia yake bandia
May 11, 2024 23:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA ya kupasisha rasimu ya azimio la kutaka kutazamwa upya suala la taifa la Palestina kupewa uanachama kamili katika umoja huo na kusema kuwa, utawala haramu wa Israel haujawahi kutengwa kwa kiwango kikubwa kama cha sasa katika historia yake bandia.
-
Afisa wa Hamas: Muqawama wa Gaza umeweza kukabiliana kwa mafanikio na vita vya dunia
May 11, 2024 23:06Sami Abu Zuhri, ambaye ni miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS), amesema kwamba Muqawama na mapambano ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamefanikiwa kukabiliana na "vita vya kimataifa," na nchi zilizoifadhili Israel sasa zinaanza kusitisha uungaji mkono wao kwa utawala huo.
-
Afrika Kusini yaitaka jamii ya kimataifa iwasaidie wananchi wa Gaza
May 11, 2024 09:14Afrika Kusini imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutoa uamuzi wa dharura wa kuwaunga mkono Wapalestina huko Rafah.
-
Kuidhinishwa rasimu ya uanachama kamili wa Palestina katika Umoja wa Mataifa
May 11, 2024 07:51Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) hatimaye limeipigia kura ya ndio rasimu ya uanachama kamili wa Palestina katika umoja huo baada ya Marekani kukwamisha suala hilo kwa miaka kadhaa.
-
Iran: Kuipa uanachama Palestina, ni hatua ya kwanza ya kukabiliana na dhulma
May 11, 2024 04:31Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Tehran inakaribisha hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA ya kupasisha azimio la kutaka kutazamwa upya suala la taifa la Palestina kupewa uanachama kamili katika umoja huo.
-
Borrell: Nchi 4 za Ulaya kulitambua taifa la Palestina
May 11, 2024 04:28Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amethibitisha kuwa nchi nne za Ulaya zitaitambua Palestina kama taifa huru.
-
Afrika Kusini yaandaa mkutano wa kimataifa dhidi ya ubaguzi wa rangi wa Israel
May 10, 2024 07:25Mkutano wa Kimataifa dhidi ya Ubaguzi wa Rangi wa Israel huko Palestina ulitazamiwa kuanza leo Ijumaa katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini na utaendelea na kazi zake hadi tarehe 12 Mei mwaka huu.
-
Al Houthi: Yemen italenga meli zenye uhusiano na Israel bila kujali zinakoenda
May 10, 2024 06:40Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdul Malik al-Houthi, amesema vikosi vya jeshi la nchi hiyo vitalenga meli za kampuni yoyote inayohusiana na kusambaza au kusafirisha bidhaa hadi Israel bila kujali zinakoelekea.
-
Iran yakosoa vitisho na mashinikizo wawakilishi wa Kongresi dhidi ya mahakama ya ICC
May 09, 2024 22:41Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa ni fedheha na jambo lenye kutia wasiwasi kuona baadhi ya wawakilishi wa Kongresi na Seneti ya Marekani wanatoa vitisho na kuwashinikiza waendesha mashtaka na majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
-
AU yailaani Israel kwa kupanua mashambulizi yake hadi Rafah
May 08, 2024 23:01Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika amelaani vikali mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.