-
Rais Rouhani: Iran na Chad zitaimarisha uhusiano wa pande mbili
Aug 12, 2017 02:26Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema nchi hii iko tayari kuimarisha uhusiano wa pande mbili na Chad katika nyuga mbalimbali.
-
Rais Rouhani: Iran ina hamu ya kustawisha zaidi uhusiano na nchi za Afrika
Aug 07, 2017 12:11Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumza kwa nyakati tofauti na Rais wa Zimbabwe na Waziri wa Utamaduni na Mawasiliano wa Senegal walioko hapa mjini Tehran na kusisitiza kuwa Tehran inataka kuimarisha zaidi ushirikiano wake na nchi hizo mbili za Afrika.
-
Rais Rouhani: Iran iko tayari kustawisha uhusiano na nchi za Afrika
Aug 06, 2017 11:54Rais Hassan Rouhani amesema mabara mawili ya Asia na Afrika yana maslahi mengi ya pamoja kwa ajili ya kushirikiana na kuongeza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa umuhimu mkubwa suala la kustawisha uhusiano na nchi za Afrika.
-
Rouhani aapishwa kuwa rais wa 7 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Aug 05, 2017 10:44Dakta Hassan Rouhani jioni ya leo amekula kiapo cha kuwa rais wa 7 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kipindi kingine cha miaka minne kwa kuahidi mbele ya Qur'ani tukufu kwamba atalinda Uislamu, Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na Katiba ya nchi.
-
Rais Mugabe awasili Tehran kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Hassan Rouhani
Aug 04, 2017 10:33Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewasili hapa mjini Tehran kuhudhuria sherehe ya kuapishwa Rais Hassan Rouhan itakayofanyika Jumamosi ya kesho.
-
Rais Rouhani: Iran haitokubali njama za maadui za kutaka itengwe kwa nguvu
Aug 03, 2017 09:42Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa pamoja na kwamba taifa hili limelipa na linaendelea kulipa gharma kutokana na azma yake ya kuwa na izza ya kujitegemea, lakini kamwe mfumo tawala wa nchi hii hautakubali njama za maadui za kutaka itengwe kwa nguvu.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi aidhinisha kura za wananchi na kumpasisha Rouhani kuwa Rais wa Iran
Aug 03, 2017 03:51Sherehe ya kuidhinisha kura za wananchi kwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu zimefanyika leo asubuhi katika Husseiniya ya Imamu Khomeini (M.A) hapa Tehran kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kumpasisha Hassan Rouhani kuwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Jumbe za zaidi ya nchi 90 kushiriki katika sherehe za kuapishwa Rais wa Iran
Aug 01, 2017 03:51Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ametangaza kuwa, kushiriki jumbe za ngazi ya juu kutoka zaidi ya nchi 90 katika seherehe za kuapishwa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakuwa ni nukta muhimu kwa ajili ya kuitangaza Iran yenye amani na uwezo.
-
Rouhani: Hakuna anayeweza kuthubutu kulidhuru jeshi la Iran
Jul 30, 2017 23:59Rais Hassan Rouhani amesema mihimili mitatu ya serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaviunga mkono kwa dhati vikosi vya jeshi la Iran na kwa msingi huo hakuna anayeweza kulidhuru jeshi hilo wala Iran.
-
Rouhani: Uwezo wa Iran umetokana na kupiga hatua katika uga wa sayansi
Jul 28, 2017 09:16Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza hatua ya Iran ya kufanya majaribio ya roketi la kupeleka satalaiti katika anga za mbali kwa mafanikio na kubainisha kuwa, mafanikio kama haya ya kisayansi ndiyo yameipa Iran uwezo na izza mkabala wa adui.