-
Rais Uhuru Kenyatta alipongeza jeshi la Kenya kwa kazi nzuri linayoifanya + Sauti
Nov 08, 2018 13:07Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amepongeza juhudi za jeshi la nchi yake KDF kujumlisha tekinolojia ya kisasa katika mfumo wake wa utoaji mafunzo kwa makuruta, akiitaja hatua hio kama chanya kwenye kuafiki kasi ya mabadiliko ya changamoto za kiusalama nchini mwake na Pembe ya Afrika. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi...
-
Bunge la Afrika lamaliza vikao vyake nchini Rwanda + Sauti
Nov 06, 2018 03:28Bunge la Afrika limekamilisha vikao vyake vya wiki mbili mjini Kigali Rwanda kwa kuanzisha tunzo maalumu ya uongozi bora barani Afrika kwa hisani ya hayati Kofi Annan, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa. Mwandishi wetu Sylvanus Karemera na ripoti zaidi...
-
Vita dhidi ya ufisadi Kenya, asasi za kijamii zaiandalia chata Serikali + Sauti
Nov 06, 2018 03:25Asasi za kijamii nchini Kenya zimeweka mikakati ya kubadilisha taswira kwenye vita dhidi ya ufisadi kwa kuandaa chata ambayo inaielekeza serikali katika kupambana na ugaidi bila ya kutumia nguvu kupita kiasi. Seifullah Murtadha na taarifa zaidi...
-
Wakazi wa Kivu Kaskazini waomboleza mauaji ya wenzao yaliyofanywa na Jenerali Nkunda Batware + Sauti
Nov 06, 2018 03:12Wakazi wa eneo moja la mkoa wa Kivu Kaskazini huko Kongo DR wamekumbuka miaka kumi tangu walipouliwa raia wenzao na wanamgambo wa Jenerali Laurent Nkunda Batware na wametaka kuundwe tume ya kuchunguza mauaji hayo. Mossi Mwassi na taarifa zaidi...
-
DRC yalalamikia uingiliaji wa Marekani katika uchaguzi wa nchi hiyo + Sauti
Nov 05, 2018 03:49Viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo wamelalamikia ripoti mpya ya Chuo kikuu cha New York cha nchini Marekani kilichodai kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwezi ujao wa Disemba huko DRC utakuwa wa hatari zaidi kuliko hata inavyotarajiwa. Mwandishi wetu Mossi Mwassi na maelezo zaidi kutoka mjini Brazzaville.
-
Raila atetea ushirikiano wake na Rais Uhuru Kenyatta Kenya +Sauti
Nov 04, 2018 03:02Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya Raila Amolo Odinga amewakosoa wale wanaosema kuwa ufanisi wake na Rais Uhuru Muigai Kenyatta kisiasa unatokana na urithi wa nasaba zao na badala yake amesisitiza ni juhudi zao endelevu kisiasa ndizo zimewapa umaarufu huo. Kwa maelezo zaidi tunajiunga na Seifullah Murtadha wa mjini Mombasa, Kenya...
-
Tamasha la kimataifa la wasoma Kasida lafanyika visiwani Zanzibar + Sauti
Nov 03, 2018 04:41Tamasha la kimataifa la Kasida limefanyika kisiwani Unguja huko Zanzibar kwa kushirikisha munshidi kutoka ndani ya Zanzibar na nje yake bali hata kutoka nchini Oman. Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya matukio ya Kiislamu iliyoandaliwa na mwandishi wetu Harith Subeit...
-
Serikali ya Kenya yawaonya vikali wanaowafanya watoto kiwanja cha mazoezi ya maovu yao + Sauti
Nov 03, 2018 04:34Serikali ya Kenya imetoa onyo kali kwa watu waovu wanaowatumia vibaya kijinsia watoto wadogo hasa wanafunzi wa shule. Maelezo zaidi anayo mwandishi wetu Seifullah Murtadha kutoka Mombasa, Kenya...
-
Wauguzi kupigwa chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Uganda + Sauti
Nov 03, 2018 04:26Wauguzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupigwa chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Uganda.
-
Wanafunzi 16,709 visiwani Zanzibar kufanya mitihani ya Kidato cha Nne mwaka huu + Sauti
Oct 31, 2018 14:27Jumla ya wanafunzi 16,709 visiwani Zanzibar wiki ijayo wanatazamiwa kufanya mitihani yao ya taifa ya Kidato cha Nne. Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit na maelezo zaidi...