Wauguzi kupigwa chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Uganda + Sauti
Nov 03, 2018 04:26 UTC
Wauguzi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupigwa chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola nchini Uganda.
Serikali ya Uganda imetangaza pia kuwa, imeazimia kuanza kutoa chanjo hiyo Jumatatu kwa wafanyakazi wake wa huduma ya afya kama sehemu ya kupambana na maradhi ya Ebola. Hatua hiyo inachukuliwa kutokana na kuongezeka wasiwasi juu ya uwezekano wa kuenea hadi Uganda homa hiyo ya kuvuja damu inayosababishwa na virusi hatari, kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo inapambana na mripuko wa Ebola. Kigozi Ismail na maelezo zaidi kutoka Kampala Uganda...
Tags