• Mahakama maalumu ya jinai yazinduliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati + Sauti

    Mahakama maalumu ya jinai yazinduliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati + Sauti

    Oct 24, 2018 02:25

    Mahakama maalumu ya jinai za kivita imezinduliwa rasmi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo ni miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani. Nchi hiyo ilitumbukia kwenye mgogoro wa kisiasa mwaka 2013 baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo François Bozizé na waasi wa Seleka. Mossi Mwasi na maelezo zaidi...

  • Vikao vya Bunge la Afrika vyaanza mjini Kigali Rwanda + Sauti

    Vikao vya Bunge la Afrika vyaanza mjini Kigali Rwanda + Sauti

    Oct 22, 2018 13:32

    Bunge la Afrika limefungua kikao chake cha wiki mbili mjini Kigali Rwanda ambapo kwa muda wa wiki mbili wabunge wake watajadili mambo kadhaa kuhusu demokrasia,uongozi bora na kurahisisha mafungamano ya biashara baina ya waafrika wenyewe. Ni kikao kilichofunguliwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.

  • Wimbi la wakimbizi wa Kongo laleta matatizo nchini Uganda + Sauti

    Wimbi la wakimbizi wa Kongo laleta matatizo nchini Uganda + Sauti

    Oct 22, 2018 13:28

    Idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanazidi kumiminika katika nchi jirani ya Uganda na kusababisha matatizo mengi ya kuwahudumia. Kigozi Ismael na maelezo zaidi kutoka Kampala

  • Kesi za uchaguzi Cameroon kuanza kusikilizwa leo Jumanne + Sauti

    Kesi za uchaguzi Cameroon kuanza kusikilizwa leo Jumanne + Sauti

    Oct 15, 2018 23:50

    Tume ya Uchaguzi ya Cameroon (ELECAM) imesema kuwa, leo Jumanne Oktoba 16, 2018 ndiyo siku ya kusikiliza kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni. Matokeo yaliyovuja ya uchaguzi wa rais yanaonesha kuwa Rais Paul Biya ameshinda uchaguzi huo wa Oktoba 7 kwa zaidi ya asilimia 71 ya kura. Mossi Mwasi na maelezo zaidi

  • Ubelgiji yakubali kuirejeshea Rwanda sehemu ya utajiri wake wa kihistoria + Sauti

    Ubelgiji yakubali kuirejeshea Rwanda sehemu ya utajiri wake wa kihistoria + Sauti

    Oct 15, 2018 23:31

    Kwa mara ya kwanza Ubelgiji imekubali kuirejeshea Rwanda baadhi ya nyaraka na turadhi za kihistoria za kabla, wakati na baada ya ukoloni. Ubelgiji ni moja ya madola ya Ulaya yaliyozikoloni kidhulma nchi za Afrika na kupora utajiri mkubwa wa nchi za bara hilo. Mwandishi wetu Sylvanus Karemera na ripoti zaidi

  • Kongamano la vijana wa Afrika mjini Kigali lazitaka nchi za Afrika kuwa na mabaraza yenye nguvu ya vijana + Sauti

    Kongamano la vijana wa Afrika mjini Kigali lazitaka nchi za Afrika kuwa na mabaraza yenye nguvu ya vijana + Sauti

    Oct 11, 2018 02:33

    Kongamano la vijana kutoka nchi zote za Afrika linatajiwa kufikia kilele chake kwa kuziomba serikali zote za bara hilo kuanzisha mabaraza ya vijana kama jukwaa la kuwasiaida vijana hao kupaza sauti zao na kujadili yale yanayowasibu. Sylvanus Karemera na ripoti kamili...

  • Miaka 56 ya uhuru wa Uganda + Sauti

    Miaka 56 ya uhuru wa Uganda + Sauti

    Oct 09, 2018 02:12

    Uganda imeadhimisha mwaka wa 56 wa uhuru wake ikiwa imetekeleza miradi mingi ya maendeleo na kufeli katika sekta nyinginezo. Taarifa kamili anayo mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismael...

  • Sheria mpya ya jinai Rwanda yapokewa kwa hisia tofauti + Sauti

    Sheria mpya ya jinai Rwanda yapokewa kwa hisia tofauti + Sauti

    Oct 03, 2018 13:23

    Mabadiliko yaliyofanywa kwenye sheria ya jinai nchini Rwanda yamepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa wadau wake katika jamii. Mabadiliko hayo ni pamoja marufuku kwa waandishi wa habari kuchora vibonzo vinavyowakashifu viongozi wa ngazi za juu akiwemo rais wa nchi .Waandishi wa habari wanahisi hilo linaloweza kusababisha wao kuwa matatani kwa njia rahisi. Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi....

  • Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi lakumbwa na malalamiko + Sauti

    Zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi lakumbwa na malalamiko + Sauti

    Oct 02, 2018 07:34

    Zoezi la kusajili vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi limekamilika katika mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja na hivi sasa linaendelea katika mkoa wa mjini Magharibi. Hata hivyo usajili huo umegubikwa na malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaodai kwamba licha ya kuwa na haki ya kusajiliwa lakini wananyimwa haki yao hiyo. Harith Subeit ametutayarishia ripoti maalumu kuhusu suala hilo...

  • Burundi waadhimisha Siku ya Makazi Dunia + Sauti

    Burundi waadhimisha Siku ya Makazi Dunia + Sauti

    Oct 02, 2018 07:05

    Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya makazi, nchini Burundi siku hiyo imeadhimishwa kwa kuhamasisha raia kukabiliana na takataka zinazotoka majumbani. Mwandishi wetu Hamida Issa na maelezo zaidi...