-
Sudan yaafiki kuanzishwa nchini humo kambi ya jeshi la wanamaji la Russia
Feb 12, 2025 23:22Khartoum na Moscow zimekubaliana juu ya kuanzishwa kituo cha jeshi la wanamaji la Russia nchini Sudan.
-
IOM: Vita vya Sudan vimeongeza idadi ya wakimbizi wa ndani Pembe ya Afrika
Feb 04, 2025 23:10Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema idadi ya wakimbizi wa ndani (IDP) katika Pembe ya Afrika iliongezeka hadi milioni 20.75 kufikia mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2024.
-
Watu 44 wauawa katika shambulio la waasi wa SPLM-N huko Kordofan Kusini
Feb 04, 2025 03:59Maafisa wa Sudan wametangaza kuwa watu wasiopungua 44 wameuawa na 28 kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa harakati ya SPLM-N inayoongozwa na Abdelaziz al Hilu katika makao makuu ya jimbo la Korofan Kusini kusini mwa Sudan.
-
Takriban watu 56 wameuawa Sudan huku mapigano yakiendelea Khartoum
Feb 02, 2025 04:07Mashambulio ya mizinga na ya anga yalisababisha vifo vya takriban watu 56 jana Jumamosi katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Haya yameelezwa na duru za hospitali na wanaharakati wa Sudan.
-
Iran yasikitishwa na shambulio la droni lililoua 70 hospitalini Darfur, Sudan
Jan 27, 2025 08:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei amelaani shambulio la ndege isiyo na rubani dhidi ya hospitali moja katika mji wa El Fasher katika mkoa wa magharibi wa Darfur nchini Sudan, na kusababisha vifo vya makumi ya watu.
-
Jeshi la Sudan ladhibiti kikamilifu kiwanda kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta nchini humo
Jan 26, 2025 03:24Jeshi la Sudan limeeleza kuwa limechukua udhibiti kamili wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha al Jaili karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum huku gavana mmoja wa nchi hiyo akiripoti kuuawa watu zaidi ya 70 katika shambulio la droni lililotekelezwa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko al Fasher magharibi mwa Sudan.
-
Jeshi la Sudan: Tumevunja mzingiro wa RSF Khartoum
Jan 25, 2025 08:05Jeshi la Sudan limetangaza habari ya kufanikiwa kuvunja 'mzingiro' uliowekwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya Kamandi Kuu ya jeshi hilo katikati mwa Khartoum, mji mkuu wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Jeshi la Sudan na RSF wapigana kuhusu kinu cha kusafisha mafuta kaskazini mwa Khartoum
Jan 24, 2025 00:06Mapigano makali yaliendelea kwa siku ya pili jana Alhamisi kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo hasimu wa jeshi hiyo yaani Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) karibu na kinu cha kusafisha mafuta kaskazini mwa mji mkuu, Khartoum.
-
Sudan: Wanamgambo wa RSF wamekishambulia kituo cha umeme cha mji wa Dongola
Jan 21, 2025 03:41Jeshi la Sudan limewatuhumu wanamgambo wa kikosi cha (RSF) kwa kukishambulia kituo cha umeme kaskazini mwa nchi hiyo na kusababisha kukatika kwa umeme katika mji wa Dongola.
-
Sudan yakosoa hatua ya Marekani ya kumuwekea vikwazo kamanda wa jeshi la nchi hiyo
Jan 17, 2025 23:11Sudan imelaani na kukosoa uamuzi wa Wizara ya Fedha ya Marekani ya kumuwekea vikwazo kiongozi wa jeshi la nchi hiyo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.