Jeshi la Sudan: Tumeuwa wanamgambo 30 wenye silaha wa RSF
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i119624-jeshi_la_sudan_tumeuwa_wanamgambo_30_wenye_silaha_wa_rsf
Jeshi la Sudan leo limedai kuwa limewauwa wapiganaji 30 wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mapigano makali yaliyozuka kati yao na kikosi hicho.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Dec 02, 2024 08:46 UTC
  • Jeshi la Sudan: Tumeuwa wanamgambo 30 wenye silaha wa RSF

Jeshi la Sudan leo limedai kuwa limewauwa wapiganaji 30 wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika mapigano makali yaliyozuka kati yao na kikosi hicho.

Jeshi la Sudan na hasimu wake yaani kikosi cha RSF wamepigana katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na katika pia katika mji wa a Fasher katika jimbo la Darfur ya kaskazini, magharibi mwa Sudan.

Watu walioshuhudia wameeleza kuwa wanamgambo wa RSF walishadidisha mashambulizi ya mizinga katika mji wa al Fasher na kuuwa watu wasiopungua watano na kujeruhi wengine kadhaa. 

RSF washadidisha mashambulizi katika mji wa al Fasher 

Wakati huo huo jeshi la Sudan limedai kuwa limesambaratisha njama ya wanamgambo wa RSF ya kutaka kuingiza silaha hatari zikiwemo droni katika mji wa al Fasher kutoka katika mji jirani wa Nyala. 

Jeshi la Sudan limesema kuwa katika mapigano ya leo na kikosi cha RSF wamefanikiwa kuuwa wanamgambo 30 wa kikosi hicho, kuwatia nguvuni kadhaa na kunasa idadi kadhaa ya silaha za adui.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF yalianza tangu Aprili mwaka jana; na hadi sasa watu zaidi ya elfu ishirini wameuawa na wengine wasiopungua milioni kumi wamekuwa wakimbizi.