-
AU yalaani jaribio la mauaji dhidi ya Waziri Mkuu wa Sudan
Mar 10, 2020 04:46Umoja wa Afrika umelaani shambulizi la bomu dhidi ya Waziri Mkuu wa Sudan, Abdulla Hamdok ambaye alinusurika kifo jana kufuatia mlipuko wa bomu uliolenga gari lake katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
-
Waziri Mkuu wa Sudan anusurika kifo katika shambulio la bomu
Mar 09, 2020 06:45Waziri Mkuu wa Sudan Abdulla Hamdok amenusurika kifo leo kufuatia mlipuko wa gari uliolenga gari lake katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
-
Yafichuka! Waziri Mkuu wa Sudan anaunga mkono kuwepo uhusiano baina ya nchi hiyo na utawala wa Kizayuni
Mar 02, 2020 22:57Msemaji wa Baraza la Utawala nchini Sudan amefichua kwamba, mazungumzo ya Mkuu wa Baraza hilo, Abdul Fattah al Burhan na Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu mapema mwezi uliopita yalifanyika kwa ushirikiano na Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Sudan.
-
Chama cha Congress cha Sudan chamtimulia mbali mwanachama wake mwandamizi kwa kutembelea Israel
Mar 01, 2020 08:39Mwanachama mmoja mwanadamizi wa chama cha Congress ya Taifa cha Sudan amefukuzwa na kumtimuliwa mbali na chama hicho baada ya kutembelea Israel.
-
PLO yaitahadharisha Sudan isifanye uhusiano na utawala haramu wa Israel
Feb 24, 2020 03:05Katibu wa Kamati ya Utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) ameitahadharisha Sudan kuhusu jitihada zake za kutaka kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Waziri Mkuu wa Sudan aunda tume ya kuchunguza ukandamizaji dhidi ya raia
Feb 22, 2020 09:11Waziri Mkuu wa Sudan ametangaza kuwa ameunda tume ya kuchunguza vitendo vya ukandamizaji vilivyofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo Alkhamisi na Ijumaa ya jana.
-
Chama cha Umma nchini Sudan chaitahadharisha serikali juu ya kufanya mapatano na Israel
Feb 17, 2020 07:57Mkuu wa Chama cha Umma cha nchini Sudan ametahadharisha kuhusiana na suala la kufanyika mapatano na utawala haramu wa Kizayuni na kubainisha kuwa jambo hilo halitakuwa na maslahi yoyote kwa serikali ya Khartoum wala kupelekea iondolewe vikwazo.
-
Vijana wa Sudan wasimulia jinsi Abu Dhabi ilivyowapeleka kupigana vita Libya
Feb 15, 2020 23:21Vijana wa Kisudan waliorejea makwao hivi karibuni wamesimulia jinsi walivyohadaiwa na kampuni ya Black Shield Security Services iliyowaahaidi kuwapa kazi za ulinzi na badala yake walijikuta wakipewa mafunzo ya kijeshi yasiyooana na kazi zao na kupelekwa bila ya kujua huko Libya na Yemen kupigana vita.
-
Sudan imekubali kuzilipa fidia familia za wahanga wa meli ya kivita ya USS Cole
Feb 13, 2020 23:10Sudan imekubali kuzilipa fidia familia za mabaharia waliouawa katika mashambulizi ya al Qaida dhidi ya meli ya kivita ya Marekani ya USS Cole miaka 20 iliyopita. Hayo yalielezwa jana na shirika la habari la Sudan, SUNA. Sudan imechukua hatua hiyo ikiwa ni katika juhudi za serikali za kuitoa nchi hiyo kwenye orodha ya nchi zinazodaiwa kufadhili ugaidi.
-
Uamuzi wa Sudan wa kumkabidhi al Bashir kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
Feb 13, 2020 00:04Wakuu wa serikali ya mpito ya Sudan hatimaye wamechukua uamuzi wa kumkabidhi rais wa zamani wa nchi hiyo kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).