Mapatano ya serikali ya Sudan na makundi ya wabeba silaha Darfur
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60580-mapatano_ya_serikali_ya_sudan_na_makundi_ya_wabeba_silaha_darfur
Serikali ya Sudan imefikia mpatano na makundi ya wabeba silaha katika eneo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa mapatano hayo, viti vinne chini ya anwani ya 'Kamati ya Amani' vitaongozewa Baraza la Mpito la Sudan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 24, 2020 23:35 UTC
  • Mapatano ya serikali ya Sudan na makundi ya wabeba silaha Darfur

Serikali ya Sudan imefikia mpatano na makundi ya wabeba silaha katika eneo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa mapatano hayo, viti vinne chini ya anwani ya 'Kamati ya Amani' vitaongozewa Baraza la Mpito la Sudan.

Kwa mujibu wa gazeti la Sudan Tribune,  kuibuka ugonjwa wa corona kumepelekea mazungumzo ya amani baina ya serikali ya Sudan na makundi wa wabebe silaha eneo la Darfur kufanyika kwa njia ya video kupitia ofisi ya Umoja wa Ulaya mjini Khartoum.

Makundi hayo ya wabebe  silaha nchini Sudan  yanafanya mazungumzo na serikali ya Khartoum chini ya mwavuli wa 'Mrengo wa Kimapinduzi wa Sudan."

Kwa mujibu wa mapatnao yaliyofikiwa,  makundi ya wabeba silaha yatapata uwakilishi katika serikali ya mpito na pia katika bunge. Walioshiriki katika kikao hicho wamesema watafikisha pendekezo hilo kwa wakuu wao na watatangaza uamuzi wa mwisho katika mkutano utakaofanyika Jumapili.

Msemaji wa uujumbe wa serikali katika mazungumzo hayo, Mohammad Hassan al-Taaishi amesema iwapo makundi ya wabeba silaha ya Darfur yataafiki pendekezo hilo, yatashirikishwa katika serikali ya mpito.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Sudan Abdalla Hamdok 

 

Wakati akiapishwa mwezi Septemba mwaka jana, Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Sudan Abdalla Hamdok alisema kuwa, serikali yake inatoa kipaumbele kwa suala la kuhitimishwa vurugu na machafuko ya ndani nchini humo na kuandaa mazingira mazuri ya kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Darfur ilikumbwa na mgogoro kuanzia mwaka 2003 uliohusisha kundi la waasi lililodai kutengwa na utawala wa Rais Omar al-Bashir aliyeng'atuliwa madarakani.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, karibu watu 300,000 waliuawa na milioni 2.5 wakalazimika kukimbia makaazi yao wakati wa mgogoro huo.