-
Jumuiya za kutetea haki za binadamu zataka sakata la kubakwa "binti" huko Tanzania lishughulikiwe ipasavyo
Aug 10, 2024 07:29Mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu yameendelea kupaza sauti yakitaka hatua za haraka zichukuliwe kuwashughulikia ipasavyo waliohusika na kitendo kiovu cha kumbaka na kumlawili binti mmoja wakidai kuwa wametumwa na "afande" kufanya ukatili huo.
-
Pezeshkian: Maingiliano makubwa ya kiutamaduni baina ya Iran na Tanzania ni fursa ya kipekee
Aug 01, 2024 06:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa maingiliano makubwa ya kiutamaduni baina ya Iran na baadhi ya maeneo ya Tanzania hasa Zanzibar, ni fursa nzuri ya kustawishwa zaidi na zaidi uhusiano wa nchi hizo mbili.
-
Viongozi wa Kiislamu Tanzania walaani vitendo vya ushoga
Jun 05, 2024 13:03Viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Tanzania wameendelea kukemea vitendo vya ushoga vinavyooenekana kushamiri katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
TZ yaitoa hofu UNHCR: Hatutafunga kambi wala kuwalazimisha wakimbizi warudi makwao
May 23, 2024 07:19Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema limepewa hakikisho na Serikali ya Tanzania kwamba kambi ya wakimbizi ya Nduta inayowapa hifadhi wakimbizi wa Burundi haitafungwa na wala wakimbizi hao hawatalazimishwa kurudi makwao.
-
Rais Samia ataka ‘waliodumisha Muungano wa Tanzania waendelee kuenziwa'
Apr 26, 2024 14:31Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania waendelee kuwaenzi na kudumisha maono ya waasisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mwl. Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume pamoja na viongozi waliofuatia baada yao, kutokana na juhudi zao za kuujenga na kuudumisha Muungano huo.
-
Majaliwa: Takriban watu 155 wamefariki dunia nchini Tanzania kutokana na mafuriko
Apr 26, 2024 03:08Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema jana Alhamisi kuwa takriban watu 155 wamefariki dunia nchini humo kutokana na mvua kubwa inayoambatana na El Nino na hivyo kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.
-
Zoezi la uokoaji laendelea Hanang huku Tanzania ikiomba msaada wa kimataifa kwa wahanga wa maporomoko
Dec 06, 2023 03:39Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiomba jumuiya za kimataifa na taasisi za ndani kusaidia juhudi za serikali ya nchi hiyo za uokoaji na kutafuta maiti wa maporomoko ya tope pamoja na misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
-
Idadi ya wahanga wa mafuriko, maporomoko Tanzania yakaribia 70
Dec 05, 2023 06:04Majanga ya kimaumbile yaliyoitikisa Tanzania yamemfanya Rais Samia Suluhu Hassan wa nchi hiyo kukatisha safari yake ya Umoja wa Falme za Kiarabu; huku idadi ya wahanga wa mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyotokea katika mkoa wa Manyara kaskazini mwa Tanzania ikiongezeka na kufikia watu 68.
-
Mafuriko na maporomoko yaua watu 47, yajeruhi 85 mkoani Manyara Tanzania
Dec 04, 2023 03:39Mkuu wa Mkoa wa Manyara ulioko kaskazini mwa Tanzania amesema, hadi kufikia jioni ya jana watu 47 walikuwa wamefariki dunia na wengine 85 kujeruhiwa wilayani Hanang mkoani humo kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.
-
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania yatoa tamko juu ya mgogoro wa Palestina
Oct 21, 2023 03:01Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanaznia Sheikh Alhaad Mussa Salim ametoa tamko kwa Umoja wa Mataifa na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kuingia kati na kusitisha vita kati ya Palestina na utawala wa Kizayuni wa Israel.