-
Upinzani wa Wamagharibi kwa usitishaji vita Gaza
Nov 14, 2023 05:53Licha ya kupita karibu siku 40 tangu ilipotokea operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa na radiamali ya utawala wa Kizayuni kwa operesheni hiyo kwa kushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza na kuuawa maelfu ya Wapalestina na uharibifu mkubwa wa eneo hilo, lakini baadhi ya madola ya Magharibi yakifungamana na Waziri Mkuu wa utawala huu, Benjamin Netanyahu, bado yangali yanapinga usitishaji wa vita hivi vya umwagaji damu.
-
"Mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza yanakanyaga sheria za kimataifa"
Nov 13, 2023 23:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran sajari na kulaani mauaji ya halaiki ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa, jinai zinazofanywa na Wazayuni katika eneo hilo lililozingira ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
-
Iran yaiambia G7: Acheni kuunga mkono mauaji ya watoto Gaza
Nov 09, 2023 23:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewakosoa vikali Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Kundi la G7 kwa kutoa taarifa ya pamoja ya kuilaani Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina (Hamas) sambamba na kuunga mkono mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Palestina yaishtaki Israel IAEA kwa kutishia kudondosha bomu la nyuklia Gaza
Nov 09, 2023 23:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amewasilisha faili mbele ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kulalamikia matamshi ya vitisho ya waziri wa utawala wa Kizayuni kwamba ikilazimu, utawala huo haramu utatumia bomu la nyuklia dhidi ya watu wa Gaza.
-
Netanyahu akataa ombi la Biden la kusitisha mapigano kwa siku 3 huko Gaza
Nov 08, 2023 22:48Rais Joe Biden wa Marekani amemtaka Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel asitishe mapigano kwa siku tatu ili kutatua suala la mateka. Kuhusiana na jambo hilo, Biden amesema katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika siku ya Jumanne alimuomba Benjamin Netanyahu asitishe mapigano ili kuandaa uwanja wa kushughulikiwa suala la mateka wa Israel.
-
Marekani na kukana mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza
Nov 07, 2023 23:11Zaidi ya mwezi mmoja umepita sasa tangu kuanza kwa vita vya Gaza na tangu kutekelezwa kwa operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" huku utawala wa Kizayuni unaoendesha operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza dhidi ya wapiganaji wa Hamas ukizidisha mashambulizi yake ya anga dhidi ya eneo hilo. Mashambulio hayo ya kinyama ya Israe; yameendelea kusababisha mauaji makubwa ya watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Gaza.
-
Iran: Vita vya maangamizi ya kizazi vya Israel vimeua, kujeruhi watu 40,000 Gaza
Nov 07, 2023 10:19Afisa wa ngazi ya juu wa haki za binadamu nchini Iran amesema vita na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza yamepelekea watu zaidi ya 40,000 kuuawa na kujeruhi.
-
Kuongezeka upinzani dhidi ya vitendo vya kijinai vya utawala wa Kizayuni katika nchi za Magharibi
Nov 06, 2023 23:01Mwezi mmoja ukiwa umepita tangu kujiri operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa na utawala wa Kizayuni kuanzisha mashambulizi makali ya mabomu ambayo hajawahi kushuhudiwa tena huko Ghaza, ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa makumi ya maelfu ya Wapalestina, wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, mwenendo wa upinzani dhidi ya vitendo hivyo vya jinai vya Israeli, umeongezeka sana duniani ikiwa ni pamoja na nchini Marekani, ambayo ni mwitifaki mkubwa wa Tel Aviv.
-
Jenerali Ashtiani: US itakabiliwa na pigo zito iwapo vita vya Gaza havitamalizika
Nov 05, 2023 23:29Waziri wa Ulinzi wa Iran ameonya kuwa, Marekani itakabiliwa na pigo kubwa na zito iwapo itashindwa kusimamisha mashambulizi ya kinyama yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
UN: Zinahitajika dola bilioni 1.2 kukidhi mahitaji ya mamilioni Gaza, Ukingo wa Magharibi
Nov 03, 2023 23:34Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imetangaza kuwa, takriban dola bilioni 1.2 zinahitajika kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya msingi ya Wapalestina milioni 2.7 katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.