"Mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza yanakanyaga sheria za kimataifa"
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran sajari na kulaani mauaji ya halaiki ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza amesisitiza kuwa, jinai zinazofanywa na Wazayuni katika eneo hilo lililozingira ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa.
Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema hayo jana katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Hungary, Péter Szijjártó na kusisitiza kuwa, jamii ya kimataifa ina wajibu wa kuzuia kutokea maafa zaidi katika ardhi za Palestina.
Ameeleza bayana kuwa: Jamii ya kimataifa inapasa kuushinikiza utawala wa Israel ili ukomeshe uvamizi wake wa kijeshi Gaza. Aidha Israel ishinikizwe ili makubaliano ya usitishaji vita wa kibinadamu na usio na masharti yatekelezwa haraka iwezekanavyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amebainisha kuwa, "Kupitia mashambulizi mtawalia ya mabomu na mauaji ya halaiki ya watu wa Ukanda wa Gaza, utawala huu (wa Israel) umekiuka wazi wazi haki zote za binadamu na sheria za kimataifa."
Kadhalika Abdollahian ametaja vitendo vya utawala wa Kizayuni katika mashambulizi yake ya kikatili ya kama kulenga shule, hospitali, ambulensi na vituo vya kutoa huduma za afya huko Ukanda wa Gaza kuwa ni jinai ya kivita.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameitaka jamii ya kimataifa mbali na kulaani ukikwaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na utawala wa Kizayuni ,lakini pia ichukue hatua za lazima ili kuhitimisha haraka na bila ya masharti mashambulizi ya utawala wa Kizayuni Gaza.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza, watu zaidi ya 11,200 wakiwemo watoto 4,630 na wanawake 3,130 wameuliwa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 hadi sasa.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Hungary, Péter Szijjártó ameeleza matumaini yake kuwa uhusiano na ushirikiano baina ya nchi yake na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utastawi zaidi katika nyuga zote zenye maslahi ya pande mbili.