-
VIDEO: Israel yatuma majasusi nchini Syria
Feb 26, 2017 23:15Kikosi maalumu cha jeshi la Israel kimeingia kwenye ardhi ya Syria kwa ajili ya kufanya ujasusi.
-
Hizbullah: Saudi Arabia inafanya juhudi za kusaidia Israel iendelee kuwepo
Feb 26, 2017 12:47Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, hii leo watu wote wameelewa wazi kwamba, Saudi Arabia inafuatilia kuwa na uhusiano na Israel na inafanya juhudi za kuusaidia utawala huo vamizi uendelee kuwepo.
-
Iran: Silaha za nyuklia za Israel ni tishio kwa usalama wa dunia
Feb 16, 2017 12:26Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, maghala ya silaha za nyukli ya utawala haramu wa Israel ni tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama wa dunia.
-
Hamas yaionya Israel isijaribu kuishambulia Ghaza
Feb 16, 2017 00:36Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel usijaribu kuichokoza na kuanzisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza.
-
Baraza la Mawaziri la Israel laidhinisha mpango wa kupiga marufuku adhana huko Quds
Feb 13, 2017 23:44Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Isarel limepasisha sheria ya kupiga marufuku kusomwa adhana katika misikiti ya Quds tukufu baada ya kuifanyia marekebisho na kisha kuirejesha bungeni.
-
Israel yaamua kuuteka kikamilifu Ukingo wa Magharibi
Feb 13, 2017 12:33Waziri wa Mazingira wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema, baada ya kutokea mabadiliko katika utawala wa Marekani na kuingia madarakani Donald Trump, wakati umefika wa kuchukuliwa hatua za haraka za kuuteka kikamilifu Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuuweka chini ya udhibiti wa Israel.
-
Darul Iftaa ya Misri yakosoa chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani
Feb 13, 2017 00:51Idara Kuu inayohusika na Fatwa za Kiislamu ya Misri (Darul Iftaa) imekosoa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani na kuchomwa moto vituo vya Kiislamu.
-
Zuma: Afrika Kusini itaendelea kuwaunga mkono watu wa Palestina
Feb 10, 2017 21:56Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amezihimiza nchi zote duniani ziendelee kuwaunga mkono na kuwatetea watu wanaokandamizwa wa Palestina.
-
Umoja wa Mataifa wakosoa ujenzi wa vitongoji vya wazayuni katika ardhi za Wapalestina
Feb 06, 2017 11:43Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amekosoa vikali kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.
-
Utawala haramu wa Israel wakiri juu ya uwezo mkubwa wa Hizbullah ya Lebanon
Feb 06, 2017 11:29Kituo cha Utafiti cha utawala haramu wa Israel kimekiri juu ya uwezo wa kijeshi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon na kueleza kuwa, uwezo wa Hizbullah uko katika kiwango cha majeshi bora ya Mashariki ya Kati.